Viongozi wa Korea Kaskazini na Korea Kusini wanatarajiwa kufanya mkutano mwezi ujao, kwa mujibu wa Korea Kusini.
Utakuwa mkutano wa kwanza wa aina hiyo kwa zaidi ya miaka 10 na wa kwanza tangu Kim Jong-un aingie madarakani nchini Korea Kaskazini.
Ujumbe huo pia ulisema Bw Kim alisema kjwa angependa kuzungumza kuhusu kuachana na silaha za nyuklia ikiwa tu atahakikishiwa usalama wa nchi yake.
Bw Kim na rais wa Korea Kusini Moon Jae-in, watakutana kwennye mpaka wenye ulinzia mkali mwezi ujao katika kijiji cha mapatano cha Panmunjom. Nchi hizo pia zilikubaliana kufungua mawasiliano ya simu kati ya viongozi hao.
Baada ya kurejea kutoka ziara hiyo isiyo ya kawaida, maafisa wa Korea Kusini walisema Bw Kim aliwaaambia kuwa hakutakuwa na majaribio ya makombora wakati mazungumzo yakiendelea.
Haya ni mabadiliko makubwa kwa kiongozi wa Korea Kaskazini kulingana na mwandishi wa BBC Laura Bicker kutoka Seoul.
Marekani inasema kuwa mazungumzo na Korea Kaskazini yataendelea tu ikiwa tu itakuwa tayari kuzungumzia suala la kuondoa silaha za nyuklia.
Wakati wa mashindano ya Olimpiki Korea Kaskazini na Kusini walionyesha urafiki kwa kutuma wanariadha kushindana kama kikosi kimoja na kufanya mazungumzo.
Lakini Marekani inashikilia msimamo wake kuwa mbinu za Korea Kaskazini zitakuwa na uzito mdogo bila ya kujitolea kwenye suala la silaha za nyuklia hasa kutokana na majaribio ya mwaka uliopita ya nyuklia na makombora yaliyofanywa na Korea Kaskazini.
Wao ni maafisa wa kwanza wa Korea Kusini kukutana naBw Kim tangu aingie madarakani. Walerejea mjini Seoul siku ya Jumanne asubuhi.
Ujumbe wa Korea Kusini unatarajiwa kuzuru Marekani baadaye wiki hii kuwajulisha maafisa wa Marekani kuhusu mazungumzo kati yao na Korea Kaskazini.
No comments:
Post a Comment