Watazamaji wataingia bure katika mchezo wa kirafiki kati ya timu ya
taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes na vijana
wenzao wa Morocco kesho Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Afisa
Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo
amebainisha hilo leo kwenye mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu
maandalizi ya mchezo huo utakoanza Saa 10:00 jioni.
Ngorongoro iliyo chini ya kocha Ammy Ninje, itakuwa na mechi mbili za kirafiki na mbali na hiyo ya kesho, nyingine itafuatia Jumatano ya Machi 21, dhidi ya Msumbiji.
Kwa Ngorongoro mechi hizo ni maandalizi ya mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la mataifa ta Afrika (AFCON U20) dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Machi 31 Uwanja wa Taifa na marudiano wiki mbili baadaye mjini Kinshasa.
Ngorongoro Heroes ipo kambini ikijiandaa na michezo hiyo miwili ya kirafiki na mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Vijana Afrika wenye umri chini ya miaka 20 chini ya Ammy Ninje ambaye pia amewahi kuifundisha Kilimanjaro Stars.

No comments:
Post a Comment