• Breaking News

    ..

    ..

    Friday, 16 March 2018

    Polisi agongwa na gari Dar es Salaam

    Askari wa usalama barabarani anayejulikana kwa jina la Sajenti Peter amegongwa na gari leo asubuhi majira ya saa 5 wakati akitekeleza majukumu yake ya kusimamia usalama barabarani jijini Dar es Salaam
     
    Mashuhuda wa ajali hiyo wameiambia EATV Saa1 kuwa, ajali hiyo imetokea katika makutano ya barabara ya Kajenge na Rose Garden eneo la Sayansi ilipokuwa akiongoza magari
    Juma Husein ambaye ni mkazi wa Sinza amesema, ajali hiyo imesababishwa na gari aina Hucher maarufu kama Daladala kushindwa kufunga breki baada ya kusimamishwa na trafiki na kisha kuligonga gari dogo aina ya Subaru ambalo lilikuwa limeruhusiwa kuondoka na kusababisha ajali iliyopelekea trafiki huyo kugongwa na gari jingine.
    Ajali hiyo imetajwa kuhusisha magari matatu, majeruhi akiwemo trafiki huyo walikimbizwa hosptali kwa matibabu zaidi, aidha Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa trafiki huyo alivunjika mkono.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI