NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Serikali imetakiwa kupanga bajeti inayotekelezeka ili kufanikisha utekelezaji wa shughuli za kimaendeleo zinazokusudiwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akitoa maazimio ya
kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa, Mwenyekiti wa Chama Cha
Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba, amesema kuwa serikali inapaswa
kupanga bajeti kulingana na matumizi halisi.
Prof.
Lipumba amesema kuwa kwa mujibu wa takwimu za Benki Kuu ya Tanzania
katika kipindi cha miezi saba kunzia julai mwaka wa jana hadi januari
mwaka huu, serikali ilipanga kutumia shilling trilioni 15.5 lakini
matumizi halisi yanakadiriwa kuwa shilingi trilioni 10.7.
Amesema
kuwa matumizi hayo ni sawa na asilimia 69 ya bajeti hiyo ambayo
utekelezaji wake unasuasua kwa katika kipindi hicho serikali ilitenga
shilingi trilioni 7.4 kwa ajili ya kutumia kwenye miradi ya kimaendeleo.
“Ni vema bajeti zetu zikawa zinazingatia hali halisi kutokana kumekuwa na matumizi madogo kuliko bajeti” amesema Prof. Lipumba.
Prof.
Lipumba ambaye ni mchumi anafafanua kuwu makadirio ya ukusanyaji wa
kodi ni mkubwa kuliko ukusanyaji halisi kwani mwezi julai mwaka jana
hadi januari mwaka huu mapato yote ya serikali yalikadiriwa kuwa
shilingi trilioni 11.7 lakini makusanyo ni trilioni 10.2 ambapo sawa na
asilimia 88.
Amesema
kumekuwa na mzunguko mdogo wa fedha (Currency in circulation) kutoka
shilingi trlioni 3.8 kwa mwezi oktoba 2015 na kufikia shilingi trilioni
3.4 april mwaka wa jana, jambo ambalo sio rafiki kwa uchumi wa nchi.
Hata
hivyo mchumi huyo ameipongeza serikali kwa juhudi za kukusanya mapato
na kutekeleza miradi mikubwa ikiwemo kujenga reli ya kisasa pamoja na
kufua umeme wa maji kwenye maporomoko.
No comments:
Post a Comment