NA TIGANYA VINCENT
RS TABORA
MKUU wa Tabora
Aggrey Mwanri amewataka wakazi wa Wilaya ya Urambo kuwa makini kwa kutoa
taarifa sahihi wakati wa zoezi la uandikishaji kwa ajili ya
vitambulisho vya Taifa ili watu wasiostahili wasije wakajipenyeza na
kupatiwa vitambulisho bila kustahili.
Akizungumza
katika Kijiji cha Ussoke Mlimani alisema kuwa wananchi wanatakiwa
kufichua watu wote wasio raia ambao wanataka kujiandikisha ili waweze
kupata vitambulisho kinyume cha sheria.
Mwanri alisema
huku nyuma Urambo katika sehemu ya Ulyankulu ilikuwa Makazi ya
wakimbikizi kutoka nchi jirani na kuongeza kuwa upo baadhi yao wakawa
wameshajipenyeza katika maeneo mbalimbali mkoani humo bila kufuata
taratibu.
Alisema ni jukumu
la kila mkazi wa Urambo ambaye ni mzalendo kufichua mbinu chafu kama
zitaka kufanyika ili kuficha ukweli wa mtu kwa makusudio ya kutaka kumpa
kitambulisho mgeni.
Mwanri alisema
ili zoezi hilo liwe na tija kwao na Taifa ni vema wananchi wakatoa
ushirikiano kwa watendaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA),
viongozi wa Wilaya wanapomtilia shaka mtu anayetaka kujiandikisha ili
uchunguzi ufanyike kuzuia udanganyifu huo.
Aidha Mkuu huyo
wa Mkoa alitoa wito kwa Wakazi wote wa Mkoa huo ambao wana sifa
kuendelea kujitokeza kwa wingi kwenda katika maeneo yalipopangwa ili
kujiandikisha kabla ya muda wa mwisho wa zoezi hilo.
Alisema kitendo
cha baadhi ya watu kupenda kujiandikisha siku za mwisho kimekuwa
kikisababisha msongamano na usumbufu kwa wananchi na kuongeza ili
kuepuka ili waende mapema vituoni.
No comments:
Post a Comment