Shirikisho la soka Barani Afrika CAF linaendelea na uchunguzi juu ya
tuhuma za kupanga matokeo (Match fixing) zinazowakabili waamuzi wa
Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Waamuzi wa Tanzania waliochezesha mchezo huo uliomalizika kwa Rayon kushinda 1-0 huko Burundi Februari 21, ni Mfalme Ally Nassoro, Frank John Komba, Sudi Idd na Israel Mkongo Mjuni ambaye alikuwa mwamuzi wa akiba.
CAF imeieleza TFF kuwa siku koja kabla ya mchezo viongozi wa timu ya Rayon wanadaiwa kufika hotelini walipokuwa waamuzi na kuingia kwenye vyumba vyao hivyo CAF inahitaji maelezo ya waamuzi kabla ya Machi 6.
Hata hivyo TFF imeweka wazi kuwa haina nia ya kumuonea mtu bali haki itatendeka na kama watabainika kuhusika wachukuliwa hatua kali. Rayon Sports ilisonga mbele baada ya kuwa imetoka sare nyumbani ya 1-1 hivyo kuwa na ushindi wa mabao 2-1
No comments:
Post a Comment