• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday 12 April 2018

    TEWW yaandaa mihtasari ya fizikia na kemia kwa elimu ya sekondari

    Taasisi ya Elimu ya watu wazima TEWW imefunga warsha ya uandaaji wa muhtasari ya fizikia na kemia iliyowashirikisha walimu wa masomo hayo kutoka baadhi ya shule za Secondary za jijini Dar es salaam.

    Akifunga warsha hiyo leo Dar es salaam kaimu mkurugenzi wa TEWW Dkt Kassim Nuhuka amesema takwimu za sensa zilizofanyika mwaka 2012 zilionyesha vijana takribani milioni tatu na nusu ambao walitakiwa wawe mashuleni awakupata nafasi ya kusoma.

     Amesema jumla ya wanafunzi 10,420 wakiwemo wanawake 6,074 (58.3%) na wanaume 4,346 (41.7%) wanaosoma elimu ya sekondari nje ya mfumo rasmi nchi nzima kwa kutumia mitaala iliyoandaliwa na TEWW.

    Aidha Dkt Nihuka amefafanua kuwa TEWW katika kuboresha utoaji wa elimu ya sekondari nje ya mfumo rasmi imekamilisha uandishi wa muhtasari ya masomo ya hisabati,biolojia,uraia.histori,jiografia,Kiswahili na kiingereza ambayo inatumika katika vituo vinavyotoa elimu ya sekondari nje ya mfumo rasmi mikoa yote nchini.

    "Ili kuwajengea wanafunzi msingi wa masomo ya sayansi hususani fizikia na kemia TEWW imeandaa mitaala ya masomo haya itakayotumika katika kutoa elimu ya sekondari nje ya mfumo rasmi na kwa sasa wanafunzi wetu wa sekondari wanasoma masomo saba likiwemo somo la baiolojia na hesabu" amesema  Dkt.Nihuka.

    Ikumbukwe kuwa TEWW ilianzishwa kwa sheria ya bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania namba 12 ya mwaka 1975 na kupewa majukumu ya kutoa elimu ya sekondari kwa njia ya ujifunzaji huria mafunzo ya jioni na kuandaa mitaala kwa ajili ya kutoa elimu nje ya mfumo rasmi.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI