• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday, 4 April 2018

    Wawekezaji waombwa kuwekeza katika uzalishaji wa ndani wa dawa

    Wawekezaji wameombwa kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya dawa nchini ili kupunguza gharama za uagizaji dawa kutoka nje ya nchi na kuchelewa Kwa dawa kuingia nchini.

    Ameyasema hayo waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu katika mkutano wa wawekezaji wenye nia ya kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba nchini.

    Mkutano huo umefanyika kufuatiwa na agizo la Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Magufuli la kutaka wakutane na wadau wa ndani hasa wawekezaji ili kuwavutia kuwekeza katika uzalishaji wa dawa na vifaa tiba.

    Pia amesema mpaka Sasa kampuni 38 tayari zimeonesha utayari katika kuwekeza katika uzalishaji wa ndani wa dawa na vifaa tiba nchini.

    Aidha amesema kwa muda mrefu wamekumbwa na changamoto ya usafirishaji dawa kutoka nje ya nchi
    kuingia nchini hivyo kupitia uwekezaji wa ujenzi wa viwanda vya dawa nchini itasaidia kupunguza changamoto hiyo kwani asilimia 94 za dawa na vifaa tiba vinanunuliwa kutoka nje na uzalishaji  dawa ndani ya nchi ni asilimia 6.

    "Dawa zinachukua muda mrefu kufika nchini inaweza kuchukua muda wa miezi 6 mpaka 9 kufika hivyo inapelekea kuwa na uhaba wa dawa"amesema Ummy.

    Pia amesema dawa kuchukua muda mrefu kufika nchini inapelekea kutumia gharama kubwa katika kulipa fedha za kuhifadhi dawa hizo.

    sambamba na hayo Ummy amesema bajeti ya dawa ya serikali imeongezeka kufikia bilioni 269,bilioni 500 ya dawa za kifua kikuu,tibii na malaria kutoka mfuko wa afya wa pamoja na bilioni 300 pia wanazipata kutoka mfuko wa afya wa pamoja  na kwa wadau wengine wanaochangia hivyo  zaidi ya tilioni moja wanatumia kila mwaka katika kuingiza dawa nchini.

    Kwa upande wa Waziri wa viwanda na uwekezaji Charles Mwijage amesema wawekezaji wawekeze katika ujenzi wa viwanda vya dawa ili kusaidia kupunguza upatikanaji wa ajira nchini.

    Pia amesema wale wote wanaohitaji kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya dawa na vifaa tiba nchini wahakikishe wanapitia katika tafiti za asasi za kiserikali.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI