• Breaking News

    ..

    ..

    Monday 28 May 2018

    Waziri Mkuu Atoa Neno Kwa Waislam Tanzania


    WAZIRI    Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasim Majaliwa Amezitaka taasisi za dini kuunga mkono juhudi za serikali katika kuendeleza elimu nchini.
    Majaliwa ameyasema hayo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika Mashindano ya 19 ya kuhifadhi kura  yaliyofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam yaliyo andaliwa na taasisi ya AL-HIKIMA FOUNDATION, ambapo ametoa wito kwa Watanzania kudumisha amani iliyopo nchi.


    "Napenda kuwaambia ndugu zangu Waislamu, tofauti za kidini hazikuanza leo, zilikuwepo tangu zamani hivyo suala la kudumisha amani ni muhimu likapewa nafasi na dini zote" amesema Majaliwa.
    Mashindano ya mwakani, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli.

    "Wakati niko hapa mbele nimepokea simu kutoka kwa Rais John Pombe Joseph Magufuli akaniuliza hao wote walio jana uwanja ni Waislam? nikamwambia ndiyo, akauli za tena nawewe ni  mgenirasmi miaka miwili mfululizo? Nika sema ndiyo, akasema  mwakani mimi nitakuwa mgeni rasmi na huyo shekh wa msikiti wa Maka nitamleta nitakuwa naye hapo" amesema  Majaliwa.
    Pamoja na hayo Waziri Mkuu Majaliwa amekabidhi zawadi kwa Washindi wa mashindano hayo.
    Mshindi wa juzuu tatu kutoka AL-HIKIMA Salah, Yasir juma  amepata zawadi ya 800,000
    Mshindi wa juzuu tano  kijana kutoka  madrasa  ya alhkima Mohamed. Ahmed zawadi milioni 1. 
    Mshindi juzuu kumi Bilal Saleh Abdalah zawadi milioni 1.2

    Mshindi Juzuu 20 kutoka Bakari Athumani kutoka Mbagala zawadi milioni 1.5 

    Mshindi  wa Juzuu 30 ni Mbwana Dadi  Abdalah kutoka pemba  kaskazini Zanzibar  katika Taasisi ya  AL-HIKIMA zawadi milion 15
    Baada ya kumalizika kwa mashindano hayo Waziri wa Dini kutoka Saudia Arabian, Dr Saleh bin Mohamad  bin Abdullah Azizi Alshekh.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI