MWENGE wa Uhuru umehitimisha ziara yake Mkoani Dar es Salaam kwa kuzinda miradi tisa yenye thamani ya sh.bilioni 3.7 , wilayani Temeke.
Mwenge uliingia moan Dar es Salaam, Julai 7 mwaka huu ukitokea Kusini Pemba, ambapo , katika Mkoa wa Dar es Salaam, jumla ya miradi 33 ilizinduliwa.
Miradi iliyozinduliwa Wilayani Temeke ni mardi wa usambazaji maji mtaa wa Mabatini, Tandika wenye thamani ya sh. Milioni 253.6.
Mradi mwingine ambeo ulikaguliwa ni wa elimu ya mafunzo ya ufundi bila malipo kwa vijana wanaoishi katika mazingira hatarishi, Kata ya Temeke, wenye thamani ya sh.milioni 4.2.
Pia Mwenge wa Uhuru, uliweka jiwe la msingi katika mradi wa ukarabati wa vyumba vya madarasa 20, ofisi mbili, maabara tatu, stoo moja, choo kimoja chenye matundu mawili katika Shule za Msingi na Sekondari ya Muungano katika Kata ya Temeke, ambapo thamani yake ni sh.milioni 489.5.
Mwenge wa Uhuru pia uliweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje la ghorofa mbili katika Kituo cha Afya Yombo Vituka, unaogharimu sh.bilioni 2.12.
Pia, ulizindua mradi wa kilimo cha kitalu na nyumba ya kijani eneo la Yombo Vituka unaogharimu sh.milioni 22.00
Mwenge uliweka jiwe la musing katika mradi wa ujenzi wa daraja kiwango cha karavati la midomo mitatu katika Mtaa wa Mashine ya Maji Kata ya Buza uliogharimu sh.milioni 685.9.
Pia, mwenge ulizindua mrafi wa uboreshaji wa mazingira na bustani ya maua kwa kikundi cha vijana cha Kwetu Pazuri, pamoja na uzinduzi wa gari ya kuzolea taka la Halmshauri ya Manispaa ya Temeke ambapo miradi hiyo imegharimu jumla ya sh.milioni 162.00
Ziara hiyo ya mbio za Mwenhe wa Uhuru iliendelea kwa kuzindua na kukagua klabu a ya kupiga vita dawa kulevya na klauw ya wapinga rush ambapo bio za mwenge zilihitimishwa kwa kukagua mapambano dhidi ya malaria, ukimwi na Kazi za kimono za vijana na anawake, Barbara ya Kilwa katika eneo la Mbagala Rangi Tatu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa miradi hiyo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Mwaka 2018, Mhandisi Charles Kabeho alipongeza viongozi wa hamashauri hiyo kwa kusimmia kikamilifu shughuli za maendeleo.
“Ninawapongeza kwa utekelezaji wa miradi hii.Serikali yetu ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. John Magufuli inaitaji maendeleo kwa wananchi wake ambapo imeweka kipaumbele katika elimu, ujenzi wa miundo mbinu na afya.Temeke mmetekeleza,”alisema Mhandisi Kabeho.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva, alisema, wamejidhatiti kuhakikisha miradi muhimu inatekelezwa kwa wakati ili kuharakisha maendeleo.
“Tunamiradi mingi inayoendelea na hai uliyozindua ni miongoni mua mirai michache tu tunayoitekeleza. Temeke tumejipanga kikailifu kuhakikisha tunaendana na quasi ya serial ya away ya tank chini ya Rais Dk. Magufuli,”alisema Lyaniva.
No comments:
Post a Comment