• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday, 2 November 2016

    SIMBA YAUSONGELEA UBINGWA,YATAFUNA KISIKI CHA YANGA NA AZAM FC


    Nahodha wa Stand United Jacob Masawe (kulia) akimzuia Ajib wakichuana vikali.
    simba-vs-stand-7
    Timu ya Simba imezamilia msimu huu kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania baada ya kuididimiza Stand United bao 1-0 mchezo uliomalizika katika uwanja wa CCM Kambarage.
    Kwa ushindi huo, unaifanya Simba SC ifikishe pointi 35 baada ya kucheza mechi 13, wakati Stand inabaki na pointi zake 22 za mechi 14 na kuwaacha watani zao wakiwa na pointi 27 tofauti ya pointi 8. 
    Simba walipata bao lao mapema kipindi cha kwanza bao hilo lilifungwa na winga machachari wa Wekundu hao wa Msimbazi, Shizza Ramadhani Kichuya kwa penalti dakika ya 33 baada ya mshambuliaji Mrundi, Laudit Mavugo kuangushwa na beki Adeyum Ahmed kwenye boksi.
    Baaada ya bao hilo, timu hizo ziliendelea kushambuliana kwa zamu, lakini ni Simba SC waliokuwa waking’ara uwanjani.
    Simba wanatarajia kurejea kesho Dar kwa ajili ya mchezo wao wa Jumamosi dhidi ya African Lyon katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
    Tazama matokeo mengine ya Mechi za Leo
    .Mbeya City 2-1 Yanga 
    .Ndanda 1-0 T.Prisons
     .Ruvu Shooting 1-0 Lyon
     .Toto 0-1 Azam FC.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI