
Wachezaji wa timu ya Mbeya Citywakishangilia goli.
Mabingwa watetezi Yanga wameangukia pua baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 toka kwa wenyeji timu ya Mbeya City mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara huu ni ushindi wa kwanza kwa Mbeya City tangu wapanda Ligi.
City walikuwa wa kwanza kupata bao likifungwa na Hassan Mwasapili baada ya kupiga faulo iliyoenda moja kwa moja na kumshinda Mlinda mlango Dida licha ya kuongoza City waliendelea kulishambulia lango la wageni kama nyuki.
Kenny Ali alipeleka kilio kwa mashabiki wa Yanga ambao walikuwa wamefurika uwanjani hapo dakika ya 36 hata hivyo kuingia kwa bao hilo kulileta mzozo mkubwa kwa mwamuzi akizongwa na wachezaji hali ambayo ilipelekea mwamuzi kulikataa bao na baadaye alikubali na mchezo kuendelea.
Dakika ya 45 Donaldo Ngoma aliifungia Yanga bap la kufutia machozi baada ya kupokea pasi nzuri toka kwa Msuva na hadi mapumziko City walikuwa wanaongoza kwa mabao 2-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kufanya mabadiliko kwa kuwatoa Mbuyu Twitte,Amis Tambwe na Deus Kaseke na kuwaingiza Geofrey Mwashiuya,Obrey Chirwa na Thabani Kamusoko hata hivyo mabadiliko hayo hayakuzaa matunda kwa mabingwa hao watetezi.
Dakika ya 80 Betra Nchimbi nusura afunge bao la tatu kwa City baada ya kuwachambua mabeki pamoja na Golikipa na shuti lake lilitoka nje hadi mwamuzi anamaliza mpira Mbeya City wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kuandika rekodi ya kwanza kuwafunga Yanga.
No comments:
Post a Comment