Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl. Herman Kapufi ameshangazwa na jitihada
binafsi zilizofanywa na wachimbaji wadogo katika kata ya Nyarugusu
wilayani hapo baada ya kushirikiana na serikali ya Kata kufanikisha
ujenzi wa shule.

Mkuu wa wilaya alifika shuleni hapo kujionea jitihada za kuboresha miundombinu ya shule ya Tologo ambayo madarasa yake yaliharibiwa na mvua zilizoambatana na upepo hali iliyopeekea kubaki darasa moja tu.

Kiongozi wa wachimbaji hao Bw. Evarist Pascal alimweleza mkuu wa wilaya kuwa kutokana na kuwepo kwa hali ambayo ilisababisha wanafunzi kusomea madarasa ambayo yalikuwa yameezuliwa na mvua walionelea ni vyema wakichangia ujenzi huo hili watoto wapate sehemu nzuri ya kujisomea.
Bw. Evarist amemwambia mkuu huyo wa wilaya kuwa ujenzi wa madarasa hayo pamoja na ofisi za walimu umegharimu kiasi cha Sh, Milioni 56 ambazo zimechangwa na wachimbaji wadogo kutoka katika machimbo ya dhahabu ya Nyarugusu.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya Mwl. Herman ameeleza kushangazwa na uzalendo ambao umeoneshwa na wachimbaji hao kwa kuchangia ujenzi wa miundombinu hiyo huku akiahidi kutoa ushirikiano kwenye ujenzi wa Zahanati ya kitongoji cha Tologo ambapo hadi sasa wachimbaji hao wamefyatua tofali 3,000
No comments:
Post a Comment