Kaimu Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja ambae ni Mkuu wa Moa wa Mjini Magharibi Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud amewataka watendaji na viongozi wa Mkoawa kaskazini kufuata falsafa za ‘hapa kazi tu na kutofanya kazi kwa mazowea zinazotumiwa na viongozi wetu wakuu wan chi ili kuimarisha upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi.
Akizungumza na katika mkutano wa tathmini hapo kwenye ukumbi wa vyuo vya amali mkokotoni ulioshirikisha wajumbe wa kamati za ulinzi na usalama,watendaji wa serikali za halmashauri za wilaya na Mkoa huo mara baada ya ziara yake ya siku 5 aliyoifanya katika mkoa wa kaskazini Unguja
Mhe Ayoub amesema amegundua kuwepo kwa kasoro na mapungufu ya kiutendaji kwa baadhi ya taasisi hizo na kupelekea kwa wananchi wengi kukosa imani na serikali yao kwa kukosa huduma muhimu hivyo,ameongeza kuwa wakati umefika kwa watendaji kuongeza kasi ya uwajibikaji ili kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi.
Kaim Mkuu wa Mkoa Kaskazini amesema wananchi wengi waliopata fursa na nafasi ya kueleza kero zao walionesha kutoridhishwa na utendaji wa watendaji hao kwa pamoja wamekubaliana kufanya kazi kwa kujituma na kupunguza kiwango cha umaskini kwa wananchi wa Mkoa huo.
Akizungumza kwa niaba ya viongozi wa Wilaya na Mkoa Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “A”Nd Hassan Ali Kombo ameahidi kuyanyia kazi kwa wakati maagizo na miongozo iliyotolewa ili kupunguza matatizo yanayowakabili wananchi wa Mkoa huo.
Akizungumza katika Mkutano huo mwenyekitin wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini unguja Nd Juma Haji amesema ameshiriki ziara hiyo kikamilifu ili kuona utekelezaji wa ilani ya chama hicho ilivyotekelezwa na serikali na kuridhishwa kwa mafanikio yaliyopatikana kufuatia ziara hiyo.
Wakati huohuo Mhe Ayoub kabla ya mkutano wa majumuisho alifanya kikao na kamati za ulinzi na usalama za Mkoa huo na kuunda kamati ndogo ya kufuatialia kero mbali mbali zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo ikiwemo suala la dawa za kulevya,udhalilishaji wa kijinsia,ajira kwa vijana,migogoro ya ardhi na watembezaji wa watalii wasio rasmini.
No comments:
Post a Comment