Na stahmili mohamed
Ikiwa ni mwezi wa kisukari duniani, ugonjwa wa kisukari
umeonekana kuwa kisababishi kikubwa cha ugonjwa wa upofu wa macho nchini
Tanzania.
Hayo yamesemwa Leo na muuguzi wa international hing
hospital catheline Chacha ambaye pia amebainisha ni kwa jinsi gani
ugonjwa huo unapelekea mtu kupoteza uwezo wa kuona.
Catheline amesema kuwa, ugonjwa wa kisukari Unasababisha
mishipa ya macho kuharibika na kuvunjika jambo ambalo hupelekea damu
kuvuja na kusababisha pazia la jicho kuhama kabisa kwenye sehemu yake
hivyo mtu kupoteza uwezo wa kuona.
"Kisukari inaharibu mishipa ya macho na kufanya mishipa
kuvunjika jambo ambalo hupelekea damu kuvuja na kusababisha pazia la
jicho kuhama kabisa kwenye sehemu yake" amesema catheline.
Pia catheline ameongeza kuwa kisukari haiharibu mishipa ya
macho peke yake bali husababisha vitu vingi sana kuharibika ndani ya
macho.
"Kisukari pia inaharibu vitu vingi sana kwenye macho na si mishipa tu" ameongeza Catherine
Mwisho amewahasa watanzania kujenga mazoea ya kutembelea
vituo vya afya Mara kwa Mara ili kujua maendeleo ya afya zao kwani ni
bora kuwahi tatizo mapema kuliko kuchelewa.
No comments:
Post a Comment