Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa PAUL MAKONDA Leo
ametangaza kiama kwa Wanaume wenye michezo ya kuwazalisha Wanawake
kisha kuingia mitini kwa kukwepa majukumu ya kulea mtoto jambo
linalosababisha ongezeko la Watoto wa Mitaani na ombaomba.
Mheshimiwa MAKONDA amesema anataka kuongezea nguvu Idara
ya Ustawi wa Jamii kwa kuuunda kamati ya Wanasheria Wabobezi kwaajili
ya kuwapeleka Mahakamani Wanaume wanaotelekeza Familia na kuwaachia
Wanawake mzigo wa Malezi.
Aidha amesema kuwa Kamati hiyo pia itafanya Marekebisho ya
Sheria ya pesa ya matunzo ya mwezi Kwa Mtoto kisha kuwasilishwa
Bungeni kwakuwa pesa inayotolewa ni ndogo na haiendani na maisha ya
sasa.
Amesema ni lazima ifike Mahala Mwanaume anaposababisha Ujauzito kwa Binti atambue analojukumu la kuhudumia.
RC MAKONDA amesema hayo wakati wa hafla ya kukabidhi
zawadi za Vifaa vya Ultrasound 10 za kisasa Aina ya "GE Vscan Access"
zenye thamani ya zaidi ya shilingi Million 150 kwa Hospital 10 zilizofanya vizuri katika kutoa huduma bora za Afya na kupunguza vifo
vya Mama na Mtoto wakati wa kujifungua.
Amezipongeza Hospital, Zahanati na Vituo vya Afya
vilivyofanikisha Mkoa wa Dar es Salaam kuwa kinara wa huduma bora za
Afya na Kupunguza Vifo vya Mama na Mtoto na kuwaasa Watoa huduma kuwa
na lugha nzuri kwa Wagonjwa.
Kwa Upande wake Mshauri Mtaalamu wa Magonjwa ya Mama na
Mtoto kutoka CRDB Dr BRENDA DIMELLO amesema Dar es Salaam imekuwa Mkoa wa kwanza kupunguza vifo vya Mama na Mtoto kutokana na usimamizi
thabiti wa RC MAKONDA na watendaji wa Afya.
No comments:
Post a Comment