• Breaking News

    ..

    ..

    Monday, 13 November 2017

    Taarifa Kuhusu soko la Hisa wiki hii

    NaStahmil Mohamed
    Thamani ya mauzo ya hisa imepanda kutoka shilingi bilioni 3 ya wiki iliyoisha Novemba3 hadi kufikia shilingi bilioni 86 kwa wiki iliyoishia novemba 10 hivyo ongezeko hili kubwa LA Mara moja limetokana na ununuzi wa hisa za TBL kwa kampuni ya SABMILLER.
    Hayo yamesemwa na  Afisa muhandamizi wa soko la Hisa bi.Marry kinabo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mauzo ya Hisa ambapo amezitaja kampuni zilizoongoza katika mauzo ya hisa ni TBL 99% ikifuatiwa na CRDB 0.56% na Voda 0.01%.
    Hata hivyo bi.Kinabo ametaja ukubwa wa mtaji wa kampuni za ndani umepanda kwa shilingi bilioni29 kutoka Trilioni 10.051 hadi kafika shilingi Trilioni 10.08 wiki hii hivyo ukubwa huu umetokana na kupanda kwa bei ya hisa ya TBL(1%).

    Katika upande wa hati fungani katika wiki iliyoishia tarehe 10 novemba yalikuwa shilingi bilioni 11.2 kutoka shilingi Bilioni 15.7 wiki iliyopita ya novemba3 hivyo mauzo hayo ya hati fungani saba za serikali zenye jumla ya thaman ya shilingi Bilioni 12.5 kwa jumla ya gharama ya shilingi Bilioni 11.2

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI