Katibu Mkuu Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Suzan Mlawi akizungumza na
Watumishi wa Wizara hiyo waliopo katika kituo cha Dar es Salaam leo
ambapo amewataka kufanya kazi kwa bidii na kufuata Sheria za Utumishi wa
Umma.
Na Anitha Jonas – WHUSM
Dar es Salaam
Katibu Mkuu Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Bi.Suzan Mlawi amewataka wafanyakazi wa
Wizara hiyo kuzingatia Kanuni Sheria na Utaratibu kwa katika kufanya
kazi.
Bi. Mlawi ametoa wito huo
alipokuwa akifanya kikao na wafanyakazi wa wizara waliyoko jijini Dar es
Salaam ikiwa ni mara yake ya kwanza kukutana na wafakazi hao baada
kuapishwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe
Magufuli.
“Ninawataka mfanye kazi kwa
kushirikiana na upendo na kila mmoja awajibike katika nafasi yake na
mhakikishe mnatoa huduma kwa wateja kwa wakati na upendo,”alisema Bibi
Mlawi.
Akiendelea kuzungumza katika kikao
hicho Katibu Mkuu huyo alitoa angalizo kwa watu wanaopenda kungangania
kazi na badae kushindwa kuzitekeleza na kusisitiza suala la uwajibikaji
ni kwa wote na kama mtu ameelemewa na kazi hana haja ya kungangania
kazi ambayo anaona hataweza kuitekeleza kwa wakati.
Naye Mwenyekiti wa TUGHE Bi
Magret Mtaki alisema wanyakazi wanaima kubwa na wewe kuwa utawasaidia
kutatua changamoto zao ikiwemo ukosefu wa vitendea kazi na mambo
mbalimbali kama ilivyoelezwa na Mkurugenzi wa Michezo
No comments:
Post a Comment