MAKAMU wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki, Javiero Rielo amemhakikishia Rais John Magufuli kuwa maandalizi ya kuanza kwa ujenzi wa bomba la mafuta la kutoka Hoima, Uganda hadi bandari ya Tanga yanaendelea vizuri na kwamba kampuni hiyo imedhamiria kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa mafanikio.
Aliyasema hayo Ikulu jijini Dar es Salaam jana alipokutana na Rais Magufuli kwa lengo la kumpa taarifa juu ya maendeleo ya maandalizi ya kuanza kwa ujenzi wa bomba la mafuta.
Mradi huo utahusisha ujenzi wa bomba lenye urefu wa kilometa 1,410 ambalo litasafirisha mafuta ghafi kutoka Ziwa Albert, Uganda hadi Tanga na unatarajiwa kuzalisha ajira za moja kwa moja 1,500 na ajira zisizo za moja kwa moja 20,000.
Gharama za mradi huo zinatarajiwa kuwa takribani Dola za Kimarekani bilioni 4 (Sh trilioni 7) na kwamba Total imesema fedha hizo zipo tayari.
Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo, Rais Magufuli alisema anaamini kuwa mradi huo utakuwa na manufaa makubwa kwa Tanzania, Uganda, Kampuni ya Total na nchi jirani.
Alisema pamoja na kwamba Tanzania ipo katika mazingira mazuri ya kutekeleza mradi huo, Serikali yake itatoa ushirikiano mkubwa ili kufanikisha mradi huo. Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amepokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi watatu wanaoziwakilisha nchi zao nchini.
Hao ni Ian Myles wa Canada, Prasittiporn Wetprasit anayeiwakilisha Thailand, Harald Gunther wa Austria. Wetprasit na Gunther makazi yao ni Nairobi, Kenya.
Hata hivyo, Rais Magufuli ametoa wito wa kuwataka waanzishe ofisi za ubalozi wao nchini. Pamoja na kuwasilisha hati zao za utambulisho, mabalozi hao wameelezea kufurahishwa na uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya nchi zao na Tanzania na kuahidi kufanya kazi bega kwa bega na serikali
No comments:
Post a Comment