SERIKALI imesema inapitia sheria iliyoianzisha Mamlaka ya Reli la Tanzania na Zambia (Tazara) ya mwaka 1995 ili pia iingizwe sekta binafsi kwa lengo la kuimarisha utendaji pamoja na kuongeza ushindani katika eneo hilo.
Mkurugenzi Msaidizi katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Aunyisa Meena alisema hayo jana jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Waziri Profesa Makame Mbarawa, wakati wa ufunguzi wa maonesho yenye kuelezea shughuli zifanywazo na Tazara ikiwa ni maadhimisho ya miaka 40 tangu kuanzishwa kwake.
Kuhusu sheria, Meena alisema hali ya Tazara inaendelea kuimarika na zipo jitihada nyingi walizozifanya ikiwa ni pamoja na kufufua injini nne walizotengeneza wenyewe ilikuongeza wigo wa kusafirisha mizigo kuelekea Kapiri nchini Zambia.
Alisema kwa sasa wataalamu wanaifanyia kazi sheria hiyo pamoja na kuwepo kwa mazungumzo yanayofanyika baina ya Serikali ya Tanzania, Zambia na China ili kuibadilisha shirika hilo na kuwa la kiushindani zaidi lenye kuongeza faida.
Alisema tangu kuanza kwa shirika hilo, lilitakiwa kusafirisha mizigo tani milioni tano kwa mwaka, jambo ambalo halijafikiwa hivyo kwa mabadiliko hayo yanayotarajiwa kiwango hicho kitaweza kufikiwa
No comments:
Post a Comment