• Breaking News

    ..

    ..

    Sunday, 28 August 2016

    JOHN BOCCO! SALUTI IBRAHIM AJIB!


    Mshambuliaji wa Simba Ibrahim Ajib (katikati) akipambana kuwatoka mabeki wa Ndanda FC
    Mshambuliaji wa Simba Ibrahim Ajib (katikati) akipambana kuwatoka mabeki wa Ndanda FC


    Jana kwenye uwanja wa Azam Complex kule Chamanzi, John Bocco alifunga mara mbili wakati Azam ikishinda 3-0 dhidi ya Majimaji. Hadi sasa ana goli tatu ndani ya mechi mbili, lakini haongelewi. Sio jana tu Bocco amendelea kuwa bora kila msimu, kufunga magoli kuanzia kumi kwa kila msimu kwake sio kazi ngumu.
    Ibrahim Ajib alifanya yake pale uwanja wa taifa, wakati Simba ilipotoka suluhu dhidi ya JKT Ruvu. Ingawa Ajib hakufanikiwa kufunga bao, lakini uwezo aliouonesha baada ya kuingia kutokea benchi kuchukua nafasi ya Muivory Coast Frederic Blagnon dakika 60 bado sio stori sana. Wadau wa soka bado tupo bize kuwasifu wachezaji wa msimu mmoja.
    Tupo bize kuwasifu maproo feki kutoka Afrika Magharibi, ambao wapo baadhi yao iwe wapo Azam, Simba au Yanga mwisho wa msimu watatupiwa mabegi yao, kama ilivyo mila na desturi la soka letu. Nina uhakika na hili subiri utaona.
    Nimewatumia Ajib na Bocco kama mfano tu kwa kile nachotaka kukisema. kila msimu wa ligi wapo wachezaji wengi wa kitanzania ambao wanakuwa kwenye kiwango bora cha uchezaji lakini bado hatuwapi heshima yao. Kama utachunguza kuna sababu moja ambayo inachangia kupuuza kile kinachofanywa na maproo wetu wa kibongo
    Baadhi ya wadau wa soka hapa nchi hatujui nini maana ya utaifa. Ndio maana mtu wa Simba hawezi kumpa heshima yake Simon Msuva kama ilivyo kwa Yanga kumsifia Ibrahim Ajib. Vilevile sio hatari sana kuhoji timu ya taifa ambao inaenda kucheza na Nigeria kuna wangapi kutoka Simba na Yanga. wakati unafanya hilo bado unaonekana unahoji kitu cha msingi
    Tanzania hatuna vipenzi vya taifa kwenye mpira tofauti na wenzetu waliotutangulia kwenye mchezo wa soka. Waingereza wote wanakuwa nyuma ya Wayne Rooney hata kama anafanya vibaya. Linapokuja suala la kumlinda Wayne Rooney kila muingereza yupo tayari kusimama nyuma yake bila ya kujali anatokea United.
    Mfano mzuri ni huu unaotokea sasa, kwenye sakata la Kipa Joe Hart dhidi ya kocha wa Man City Pep Guardiola. Kila Muingereza hakubaliani na kile anachokifanya Pep Guardiola kutaka kumuacha Hart, sababu ni utaifa tu.
    Sisi hatupo tayari kuiga mazuri kutoka kwa wenzetu. Sasa ifike wakati wa kuthamini kile wanachofanya kina Ajib, Bocco  kwenye kila msimu wa ligi kuu ya Vodacom. Hawa watu wana uwezo wa kukupa mabao angalau kuanzia kumi kwa msimu, kupitia kazi ya miguu yao.  kwa nini tusiwape heshima yao?  Tusipuuzie sababu wana passport ya Tanzania. Saluti kwao

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI