• Breaking News

    ..

    ..

    Sunday, 28 August 2016

    YANGA YAANZA VPL KWA KUCHUKUA POINTI 3 KWA AFRICAN LYON

    Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania bara Yanga SC wameanza vizuri msimu mpya wa waligi kwa kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya African Lyon iliyopanda daraja msimu huu.
    Donald Ngoma akichuana na Hamad Jafari
    Donald Ngoma akichuana na Hamad Jafari
    Mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma akimtoka beki wa African Lyon Hamad Tajiri
    Mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma akimtoka beki wa African Lyon Hamad Tajiri
    Mchezo wa leo (August 28) ni mchezo wa kwanza kwa Yanga ambao walishindwa kuanza ligi juma lililopita kutokana na kukabiliwa na mchezo wa kimataifa kombe la shirikisho Afrika hatua ya makundi dhidi ya TP Mazembe mechi iliyochezwa Lumbumbashi, DR Congo.
    Simon Msuva (kushoto) akijaribu kumtoka Omar Salum wa African Lyon
    Simon Msuva (kushoto) akijaribu kumtoka Omar Salum wa African Lyon
    Magoli ya Yanga yamefungwa na Deus Kaseke aliyefunga bao la kwanza dakika ya 20 kipindi cha kwanza huku Simon Msuva akiifungia Yanga bao la pili dakika ya 60.
    Juma Mahadhi aliyetokea benchi aliifungia Yanga bao la tatu dakika ya 90+4 na kuihakikishia Yanga pointi tatu za kwanza katika mchezo wake wa kwanza huku ikiwa haijaruhusu goli.
    IMG_0075
    Ushindi kwa upande wa Yanga ni mwanzo mzuri katika mbio zao za kutetea taji la VPL msimu huu ambapo msimu uliopita walifanikiwa kutetea taji hilo kwa kulitwaa kwa mara ya pili mfululizo chini ya kocha Hans van Pluijm.
    IMG_0044
    Baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1 na Azam FC kwenye mchezo wao wa kwanza wakiwa ugenini Azam Complex, African Lyon imeendelea kucheza ugenini mchezo wao wa pili
    Yanga: Deogratius Munishi, Hassan Kessy Ramadhani , Vicent Andrew, Vicent Bosou, Mwinyi Haji, Simon Msuva/Juma Mahadhi, Thaban Kamusoko, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke/Yussuf Mhilu, Amis Tambwe, Donald Ngoma/Matheo Anthony.
    African Lyon: Youthe Rostand, Halfan Twenye, Hamad Tajiri, William Otong, Baraka Jafari, Omary Abdallah, Hood Mayanja, Tito Okello.
    Matokeo ya mechi ya CCM Kirumba, Mwanza
    Mchezo mwingine wa ligi kuu Tanzania bara ulichezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba mwanza kati ya Toto Africans dhidi ya Mbeya City mchezo ulioshudia Toto kichapwa kwenye uwanja wake wa nyumbani kwa goli 1-0.
    Bao pekee katika mchezo huo limefungwa na Haruna Shamte mchezaji wa zamani wa Toto Africans ambaye kwa sasa anakipiga kwa wagonga nyundo wa jiji la Mbeya.


    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI