POLISI mkoani Shinyanga imeeleza kuwa mauaji ya vikongwe yameendelea kutokea mkoani humu ambako katika kipindi cha Januari mwaka jana hadi Agosti mwaka huu, vikongwe 26 waliuawa kutokana na imani za kishirikina miongoni mwa jamii.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa huu, Muliro Jumanne Muliro, aliyasema hayo kwenye kikao cha viongozi wa dini kilichoitishwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainabu Telack mjini hapa.
Alisema katika kipindi cha Januari hadi Desemba mwaka jana, vikongwe 20 waliuawa kutokana na imani za kishirikina ambapo kati yao 15 walitoka wilayani Shinyanga, watatu kutoka Kishapu na wawili kutoka Kahama.
Alibainisha kuwa kwa kipindi cha Januari hadi Agosti mwaka huu, vikongwe sita waliuawa mkoani hapa, kati yao watatu kutoka wilayani Shinyanga na wengine watatu kutoka katika Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama
No comments:
Post a Comment