• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 25 August 2016

    Leteni taarifa hatua mlizochukua dhidi ya wafujaji fedha za Tasaf’



    WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene, ametoa siku sita kwa serikali za mikoa kuwasilisha taarifa kuhusu hatua zilizochukuliwa dhidi ya watumishi wa serikali waliosababisha matumizi mabaya ya fedha kwa kuwaingiza walengwa wasiostahili kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, unaoendeshwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf).
    Alitoa agizo hilo kupitia hotuba yake iliyosomwa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, aliyemwakilisha kufungua mkutano wa siku mbili wa kazi wa wakuu wa mikoa, makatibu tawala, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa Mamlaka wa Serikali za Mitaa wa mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa, Ruvuma na Songwe.
    Alitaja changamoto zinazoukabili Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (Tasaf III) kuwa ni pamoja na kuingizwa kaya zisizo na sifa, kuachwa kwa kaya ambazo ni masikini zaidi na familia za viongozi kuingizwa kwenye mpango.
    Nyingine ni kutofikisha ruzuku stahiki kwa walengwa wa mpango kutokana na baadhi ya watumishi wa umma au wasimamizi wasio waaminifu kupunguza malipo kwa walengwa, kuchukua malipo ya walengwa waliofariki au kuhama kutoka kwenye maeneo yao na baadhi ya walengwa kutofika wao wenyewe kupokea fedha na badala yake wengine wamekuwa wakichukuliwa fedha kitu ambacho si utaratibu.
    Alisema wapo viongozi wa Kamati za Mpango ambao nao wamejiweka kuwa sehemu ya walengwa, jambo alilosema kuwa haliruhusiwi.
    Alisema kutokana na utekelezaji wa agizo la Tamisemi kupitia Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora la Februari, 2016 la kufanya uhakiki wa kaya zilizopo kwenye mpango huo ili kuziondoa zisizo na sifa, hadi sasa kaya 32,456 zimeondolewa kwenye mpango huo.
    Alisema kati ya kaya hizo 9,342 ni za watu wasiofahamika na kutojitokeza 8,348 ni za wasio na sifa 7,819 ni za waliofariki, 2,999 ni za viongozi na kaya 3,948 ni za waliohama sehemu ambao mpango haujaanza.
    “Naomba kusisitiza zoezi hili ni endelevu na lazima kusimamia utaratibu wa kutoa taarifa kwa walengwa ambao wamefariki au wamehama ili fedha za serikali zisitumike hovyo nje ya malengo yaliyokusudiwa,” alisema.
    “Kwa watumishi ambao wamesababisha matumizi mabaya ya fedha hizo au kuwaingiza walengwa wasiostahili, ofisi yangu imeelekeza kupatiwa taarifa ili kujua hatua zilizochukuliwa dhidi yao kwa lengo la kukomesha tabia hizo. Na nataka taarifa hizo zifike ifikapo Agosti 30,” alisisitiza na kuongeza kuwa utekelezaji wa Tasaf III umewafikia walengwa wapatao 6,500,000 katika kaya masikini na zinazoishi kwenye mazingira hatarishi zaidi ya 1,100,000

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI