• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 25 August 2016

    Vitabu vya la nne hadi la saba kuhakikiwa ubora



    WIZARA ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi imewaagiza wachapishaji wa vitabu vya darasa la nne hadi la saba vyenye Ithibati ya Vitabu na Vifaa vya Kielimu (EMAC), kuvipeleka kwa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), ili vitathminiwe kabla ya Septemba 30, mwaka huu.
    Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali cha wizara hiyo ilisema kuwa Waraka Namba 4 wa mwaka 2014 umeipa TET mamlaka ya kufanya udhibiti wa ubora wa vitabu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia.
    Taarifa hiyo ilisema, tathmini hiyo inafanywa ili kuhakiki vitabu hivyo kwa kuwa mitaala imeongezewa vitu vipya ambavyo inataka kuhakikisha kuwa vimo katika vitabu hivyo au la.
    Ilisema pia kuwa tathmini hiyo imelenga kuvifanya vitabu hivyo viendane na wakati uliopo kwa kuwa aina inayotumika kwa vitabu hivyo ni tofauti na havifanani.
    Kwa mujibu wa taarifa hiyo, vitabu vingine vina kasoro ya kiuandishi, ndio maana wizara imeagiza vihakikiwe upya.
    Ilisema, “Ili kufanikisha zoezi hilo, nakala nne za kila chapisho ziwasilishwe kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania kabla ya Septemba 30, mwaka huu. Ilisema baada ya muda huo, vitabu vitakavyokuwa havijafikishwa kwenye taasisi hiyo kuhakikiwa vitafutwa kwenye orodha ya vitabu vyenye ithibati

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI