• Breaking News

    ..

    ..

    Saturday, 20 August 2016

    Serengeti Uwanjani leo



    KOCHA Mkuu wa timu ya soka Taifa ya Vijana waliochini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ Bakari Shime amesema kuwa amemaliza kazi yake kwenye timu hiyo na kilichobaki ni kwa mashabiki kufika kwa wingi kuishangilia leo.
    Akizungumza na gazeti hili jana, Shime alisema anaamini shabiki ni mchezaji wa 12 uwanjani hivyo anawaomba kufika kwa wingi kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Afrika Kusini utakaochezwa Uwanja wa Chamazi, Mbagala.
    “Vijana nimewandaa na naamini tutashinda mchezo huo lakini nawasihi mashabiki kufika kwa wingi uwanjani kwa ajili ya kuishangilia timu yao”, alisema Shime kwa kujiamini.
    Naye kocha wa Amajimbos ya Afrika Kusini, Rory Minnaar alisema wamekuja kwa kazi moja ya kuhakikisha wanatetea vyema bendera ya Afrika Kusini ila joto linawatatiza

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI