• Breaking News

    ..

    ..

    Saturday, 20 August 2016

    Waziri afafanua rufaa kupinga ndoa za utotoni



    WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kuwa anaunga mkono hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kupinga ndoa za utotoni.
    Alisema wadau wengi wamekuwa wakishangaa kwa nini serikali imeamua kukata rufaa kupitia hukumu hiyo iliyotolewa Julai 8, mwaka huu ya kwamba umri sahihi wa mtu kuolewa ni kuanzia miaka 18.
    Akizungumza katika uzinduzi wa awamu ya pili ya Mradi wa Kulinda Haki za Wasichana nchini, Mwalimu alisema serikali ilipokata rufaa watu wengi walikuwa wakijiuliza kuwa huenda serikali inataka kuendelea na vifungu vya kisheria vinavyoruhusu watoto wa kike kuolewa chini ya umri wa 18

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI