• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday 31 August 2016

    TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

    POLISI
    POLISIJeshi la Polisi mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo ya ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana na wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu na kumakata mali mbalimbali.
    Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya mnamo tarehe 14.08.2016 hadi tarehe 30.08.2016 lilifanya misako mbalimbali katika maeneo ya Jiji la Mbeya. Misako hiyo ilifanyika maeneo ya Mwanjelwa, Soweto, Isanga, Airport, Uyole, Sae, Nzovwe, Forest Mpya, Mama John, Ilomba, Iwambi, Iyunga na Sinde. Katika Misako hiyo iliyolenga kukomesha vitendo vya wizi na uvunjaji nyumba wakati wa usiku na mchana, mali na vitu mbalimbali vya wizi vilipatikana pamoja na watuhumiwa 05 kukamatwa kuhusika katika matukio hayo na watuhumiwa wengine 19 waliouziwa mali za wizi.
    Mafanikio yaliyopatikana katika misako:
    KUPATIKANA NA SARE YA JESHI [JWTZ]
    Mnamo tarehe 28.08.2016 majira ya saa 14:30 mchana huko maeneo ya Iwambi Jijini Mbeya, Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la MUSA ASWILE (39) Mkazi wa Iwambi alikamatwa akiwa amevaa mkanda wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)
    Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.
    KUPATIKANA NA NOTI BANDIA.
    Mnamo tarehe 30.08.2016 majira ya saa 09:00 asubuhi huko Mtaa na kata ya Sinde, tarafa ya Sisimba, Jijini Mbeya, Mtu mmoja mkazi wa Mama John aliyefahamika kwa jina la DAIMON ISACK (30) alikamatwa akiwa na noti bandia 30 za Tshs 10,000/= sawa na Tshs 300,000/= zenye namba BT-4628546 noti 2, BT 4628547 noti 2, BT 4628550 noti 7, BT 4628553 noti 3, BT 4628555 noti 2, BT 4628560 noti 6, BT 4628561 noti 6 na BT 4628562 noti 2. Upelelezi unaendelea-.
    Mnamo tarehe 28.08.2016 majira ya saa 00.01 usiku huko Uyole Jijini Mbeya, Mtu mmoja mkazi wa Itezi Uyole aliyefahamika kwa jina la MAWAZO JAMES (34) alikamatwa akiwa na noti bandia sita (06) za Tshs. 10,000/= zenye jumla ya thamani ya Tshs. 60,000/= zikiwa na namba FM-1629254 noti 03 na FH-0207276 noti 03. Mtuhumiwa alikamatwa wakati anataka kuwekewa fedha hizo kwenye simu yake akiwa kwenye kibanda cha M-PESA. Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.
    Kupatikana kwa Mali za Wizi: Katika misako hiyo, mali na vitu mbalimbali vya wizi vilipatikana ambavyo ni:-
    1. Laptop moja aina ya Dell
    2. Laptop moja aina ya Toshiba
    3. Laptop moja aina ya HP
    4. Laptop moja aina ya Inspiwn
    5. Flat Screen moja aina ya LG Inchi 50
    6. Flat Screen moja aina ya Samsung Inchi 48
    7. Flat Screen moja aina ya Home Base Inchi 24
    8. Flat Screen moja aina ya Singsing Inchi 24
    9. Flat Screen moja aina ya TCL
    10. TV aina ya Pine Tech Inchi 04
    11. Flat Screen aina ya Samsung Inchi 38
    12. TV aina ya Pine Tech Inchi 21
    13. Mixer moja aina ya Omax
    14. Speaker kubwa mbili zisizokuwa na majina
    15. Subwoofer tatu aina ya Sea Piano na Speaker mbili
    16. Subwoofer moja aina ya Tech Sonica na Speaker zake
    17. Subwoofer moja aina ya Rising
    18. Booster moja
    19. Subwoofer mbili aina ya Bass na Speaker zake nne
    20. Subwoofer moja aina ya Aborder na Speaker zake mbili
    21. Subwoofer moja aina ya Rising
    22. Deck mbili aina ya Singsung
    23. Deck moja aina ya LG
    24. Speaker moja ndogo isiyo na jina
    Aidha vitu vingine vilivyopatikana ni pamoja na hot pot mbili kubwa, hamittom reach moja aina ya Toster, sufuria moja, tablet moja aina ya Vodafone, Simu ya mkononi aina ya Nokia 215, Blender machine moja, camera aina ya Jenopiticl pamoja na mafuta ya kula lita 07.
    Kukamatwa Watuhumiwa 05 wa Uhalifu sugu: Aidha katika misako hiyo watuhumiwa 05 walikamatwa na kukiri kuhusika katika matukio ya wizi na uvunjaji wa nyumba usiku na mchana na kuiba ambapo majalada ya uchunguzi yalifunguliwa. Watuhumiwa hao ni pamoja na:-
    1. ISRAEL YOHANA (16) Mkazi wa Ilolo
    2. JUMA SIMONI (17) Mkazi wa Isanga
    3. FRANK MDENDEMI (18) Mkazi wa Kabwe
    4. YOHANA MFILINGE (17) Mkazi wa Uyole
    5. LAZARO GODWIN (22) Mkazi wa Mwanjelwa
    Aidha watuhumiwa wengine 19 waliouziwa mali za wizi walikamatwa katika misako hiyo ambao ni:-
    1. HUSEINA GADAU (55) Mkazi wa Mama John
    2. JERRY EVARIST (29) Mkazi wa Isanga
    3. SAID RASHID (18) Mkazi wa Soweto
    4. GWANDILO AMNONI (28) Mkazi wa Isanga
    5. MATOKEO JOSEPHAT (36) Mkazi wa Ilemi Darajani
    6. ANGANISYE KANYITA (46) Mkazi wa Makunguru
    7. HAPPY MASHAKA (22) Mkazi wa Makunguru
    8. FARAJA FREDY (23) Mkazi wa SIDO
    9. DONARD VERINACH (18) Mkazi wa Airport
    10. MAHMOOD MAKOPA (21) Mkazi wa Soweto
    11. BONLISE JASTIN (26) Mkazi wa Pambogo
    12. FURAHA CHAULA (25) Mkazi wa Mafiati
    13. ADAM JOHN (24) Mkazi wa Soweto
    14. BENJAMIN BUKUKU @ BEN (25) Mkazi wa Uyole
    15. MARIAM MWAKAMELE (23) Mkazi wa Manga
    16. MATHEW ANGELILE (25) Mkazi wa Makunguru
    17. PETER MWAMAFUPA (22) Mkazi wa Ilemi
    18. HENRY MWAMFUPE @ ENULE (24) Mkazi wa Mama John
    19. BRAITON SHABAN (22) Mkazi wa Soweto
    Aidha katika zoezi hilo la Misako lilienda sambamba na ukaguzi wa nyumba za kulala wageni zilizopo katika maeneo ya Uyole, Sae, Airport, Mama John, Forest ya Zamani, Ilomba, Iyunga, Forest Mpya, Mwanjelwa, Block T, Kabwe, Makunguru na Jua Kali. Hali kadhalika wamiliki na wahudumu katika Nyumba hizo za kulala wageni walipewa elimu ikiwa ni pamoja na kuandika majina ya wageni wote katika kitabu cha wageni pamoja na kuweka namba za wahudumu, wamiliki na viongozi wa Jeshi la Polisi kwenye milango kwa ajili ya dharura zitakazojitokeza kwa hatua zaidi.
    WITO:
    Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishna wa Polisi DHAHIRI A. KIDAVASHARI anatoa wito kwa jamii hasa vijana kuacha tabia ya kutaka kupata mali au utajiri kwa njia ya mkato na badala yake wafanye kazi halali ili wapate kipato halali. Pia anasisitiza kuwa maendeleo hayapatikani kwa kufanya kazi hama biashara haramu, watumie fursa zilizopo Mkoa wa Mbeya kujitafutia ajira. Aidha anatoa wito kwa wakazi wa Mbeya walioibiwa vitu vyao kufika kituo cha Polisi Kati (Central Police Station) kwa ajili ya utambuzi wa mali zao.
    Imesainiwa na:
    [DHAHIRI A. KIDAVASHARI – DCP]
    KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI