• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday 31 August 2016

    TANAPA KUTUMIA TUKIO LA KUPATWA KWA JUA KUFUNGUA LANGO LA PILI LA KUINGIA RUAHA NATIONAL PARK.

    Mkuu wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya ,Reuben Fune akiangalia jua kwa kutumia kifaa
    maalum ambacho kinachuja mwanga ili usiweze kuathiri macho kifaa hicho
    kitatumika katika tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kutokea Septemba mosi .Kushoto ni mnajimu
    Dkt Noorali Jiwaji akimuelekeza namna ya kukitumia.
    Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa)  Pascal Shelutete
    akizungumza na wanahabari wilayani Mbarali (hawapo pichani) namna ambavyo Tanapa ilivyo jipanga na tukio la kupatwa kwa jua   litakalotokea Septemba mosi. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mbarali , Reuben Fune
    Mtaalam wa masuala ya anga (Mnajimu) Dkt Noorali Jiwaji akizungumza na waandishi wa
    habari wilayani Mbarali mkoani Mbeya kuhusu maandalizi na uwepo wa vifaa vya
    kuangalizia jua wakati wa tukio la kupatwa litakalotokea Septemba Mosi.
    Mahema yakiwa yameanza kuwekwa katika eneo la Mpunga Relini ,Rujewa wilayani Mbarali,eneo lililotengwa maalum
    kwa ajili ya kutizamia tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kutokea
    Septemba mosi .
    Eneo la Mpunga Relini ,Rujewa wilayani Mbarali,eneo lililotengwa maalum
    kwa ajili ya kutizamia tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kutokea
    Septemba mosi . 
     
    Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Mbarali,Mbeya . 
     
    SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limetangaza kutumia tukio  la kupatwa  kwa jua
    linalotarajia kuonekana Septemba mosi  mwaka huu kufungua lango la Ikoga
    katika wilaya ya Mbarari mkoani Mbeya ili kuongeza watalii katika HIFADHI
    ya Taifa ya Ruaha 
    Kufuguliwa kwa lango hilo kunafanya idadi ya milango ya
    kuingilia katika hifadhi hiyo kufikia miwili ukiacha lango kuu la Way Junction
    ambalo limekuwa likitumika kwa muda mrefu sasa
    Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)
    Pascal Shelutete  anasema kuongezeka kwa
    geti la Ikoga ni  fursa kubwa ya
    kuhamasisha utalii wa ndani kwa kuwa  eneo la Ihefu
    linakivutio kikubwa cha wanyama
    wa aina mbalimbali .
    Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Ndiza Mfune, anasema
    Wilaya hiyo   ina vivutio vingi, hivyo
    amewataka  wananchi watakaofika kuangalia
    kupatwa kwa jua hiyo Septemba Mosi , kutumia fursa hiyo kutembelea vivutio
    vilivyopo Wilayani humo.
    Tukio la kupatwa kwa jua linategemea kutokea Septeba mosi
    majira ya nne asubuhi hadi saa nane mchana katika kata ya Rujewa eneo la Mpunga
    Relini Kiometa 3.5 kutoka barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam kueleka Mbeya .

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI