• Breaking News

    ..

    ..

    Tuesday, 23 August 2016

    Utendaji TRL wamridhisha waziri

    Image result for kigoma tanzania

    WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango ameeleza kuridhishwa na utendaji wa Shirika la Reli nchini (TRL) na kusema kuwa serikali inaendelea na mpango wake wa kuimarisha reli hiyo ili iweze kuleta tija kwa uchumi wa nchi na maisha ya Watanzania.
    Akizungumza katika ziara yake mkoani Kigoma, Dk Mpango alisema kwa sasa TRL inafanya kazi zake kwa ufanisi kwa kuwepo na usafiri wakati wote lakini pia kuwa na makusanyo ya kutosha ya mapato ya serikali katika mizigo na abiria.
    Alisema Mkurugenzi wa TRL, Masanja Kadogosa ameweza kusimamia maelekezo ya serikali ya kulinyanyua kimapato shirika hilo, kazi ambayo ameianza vizuri na serikali iko mbioni kujenga reli mpya ya kisasa.
    Alisema ujenzi huo pamoja na ubunifu wa mkurugenzi huyo litaifanya reli hiyo kufanya kazi kwa tija na kutimiza lengo la serikali la reli hiyo kuwa kiungo muhimu katika kuinua uchumi wa nchi.
    “Kwa kiasi kikubwa treni yetu ilikuwa kama shamba la bibi unaona treni imejaa lakini hakuna mapato ya kutosha kwa serikali, tumeondoa hilo na sasa serikali inakusanya mapato ya kutosha kupitia treni zetu,tunataka watendaji kama huyo Mkurugenzi wa TRL ambaye anafanya kazi aliyotakiwa kufanya,” alisema.
    Sambamba na hilo aliwataka watendaji wa Idara ya Takwimu kufanya utafiti kujua kiwango halisi cha mizigo na shehena kinachohudumiwa na bandari ya Kigoma, akieleza kutoridhishwa na taarifa za tani 126 kwa mwaka zinazohudumiwa na bandari hiyo yenye uwezo wa kuhudumia shehena tani 600.
    Katika hatua nyingine , Waziri huyo ametaka kuwepo kwa ufanisi katika matumizi ya fedha za serikali zinazopelekwa kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali ili kuondoa ujanjaujanja na matumizi ya fedha yanayofanya miradi kutekelezwa chini ya viwango.
    Awali Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Emmanuel Maganga akisoma taarifa yake alisema kuwa huduma za TRL zimeendelea kuimarika na wananchi kutumia huduma hizo kwa ufanisi kwa shughuli mbalimbali ikiwemo shughuli za kiuchumi.
    Maganga alisema ili kuondoa malalamiko ya wananchi ya ulanguzi wa tiketi, TRL imeamua kufungua vituo vya kuuzia tiketi katika wilaya za Kasulu na Kibondo ambako wananchi wake kwa kiasi kikubwa walikuwa waathirika kwa vitendo vya kuuziwa tiketi za treni kwa bei ya ulanguzi.
    Alisema Sh milioni 368.2 zimerudishwa na waliokuwa watumishi hewa wa serikali mkoani humo, ambapo watumishi hewa 247 walibainika na Sh bilioni 1.4 bado zinadaiwa kwa watumishi hao

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI