WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewaomba viongozi wa dini, wawe wanawaelimisha waumini wao umuhimu wa kulinda amani na kuishi kwa kufuata sheria na taratibu za nchi husika.
Alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza na waliokuwa wakimbizi wa Burundi, ambao kwa sasa wamepewa uraia wa Tanzania wanaoishi katika kata ya Katumba, Halmashauri ya Nsimbo wilayani Mpanda.
Katika hatua nyingine, amesisitiza kwamba wakimbizi waliopewa uraia wa Tanzania na kuitumia vibaya nafasi hiyo kwa kuingiza watu wengine kinyume cha sheria watanyang’anywa na kurudishwa walikotoka.
Waziri Mkuu alisema lazima ulinzi uimarishwe katika maeneo ya mipakani na wasipofanya hivyo, watu wengi wataingia nchini bila ya kuwa na vibali hivyo kusababisha ongezeko kubwa la idadi ya watu.
Kuhusu viongozi wa dini, alisema, viongozi hao wana wajibu mkubwa wa kuwaelimisha waumini wao umuhimu wa kulinda amani na kuishi kwa kufuata sheria na taratibu za nchi husika.
Wakati huo huo, Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda wasiwaudhi wakulima na wafanyabiashara wadogo kwa kuwatoza ushuru kwenye mazao wanapotoka shambani kama debe moja la nafaka na wanaouza bidhaa ndogo ndogo.
“Mkulima ametoka shambani na debe moja la mahindi unamtoza ushuru maana yake nini? Halmashauri tusitafute mgogoro katika hili. Tafuteni biashara za kutoza ushuru. Mkulima anatoka kijiji cha Kanoge anakwenda kijiji cha Ikongo ushuru wa nini?” Waziri Mkuu alihoji. “Tumewasisitiza mkusanye kodi lakini si hivyo. Mkiendelea kutoza ushuru kwa wakulima wanaotoka shambani na mahindi kidogo mtasababisha wakate tamaa ya kulima,” aliongeza Waziri Mkuu.
Akisoma taarifa ya maendeleo ya mkoa wa Katavi juzi jioni baada ya Waziri Mkuu kuwasili mkoani Katavi, Mkuu wa Mkoa, Meja Jenerali mstaafu Raphael Muhuga alisema mkoa una jumla ya wakimbizi 6,918 wanaoishi katika kambi za Mishamo na Katumba ambapo kati yake wakimbizi 2,150 waliomba uraia wa Tanzania na kunyimwa
No comments:
Post a Comment