• Breaking News

    ..

    ..

    Monday, 22 August 2016

    Wanaotorosha kahawa usiku Mbinga wasakwa


    Image result for mbingaHALMASHAURI ya wilaya ya Mbinga imeanza kuwasaka wafanyabiashara wajanja wanaonunua na kutorosha kahawa wilayani humo nyakati za usiku kwa njia za panya kwenda mkoani Mbeya, bila kibali maalumu.
    Halmashauri hiyo imebainisha kuwa vitendo hivyo vimekuwa vikishamiri hasa kipindi hiki cha kiangazi, pale msimu wa mavuno ya zao hilo unapofanyika na wafanyabiashara hao hupita vijijini kwa wakulima na kuwarubuni kununua zao hilo kwa njia zisizo halali.
    Mkuu wa wilaya ya Mbinga, Cosmas Nshenye alisema hayo juzi alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya hiyo, lililoketi mjini hapa.
    “Tunafanya msako mkali sasa wa kuwakamata watu wote wenye tabia hii, mfanyabiashara atakayekamatwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa ikiwemo kufutiwa hata leseni ya kununua zao hili katika msimu huu”, alisema Nshenye.
    Aidha, alikemea biashara za magoma ambazo zimekuwa zikifanywa katika maeneo mbalimbali wilayani Mbinga, ambapo wafanyabiashara hao wamekuwa wakimrubuni mkulima anayezalisha zao hilo, kabla ya kahawa yake kuvunwa shambani kwa mtindo wa kubadilishana na bidhaa mbalimbali.
    Mkuu huyo wa wilaya aliahidi kuwa atakayekamatwa atachukuliwa hatua za kisheria, pamoja na kufikishwa mahakamani ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI