• Breaking News

    ..

    ..

    Monday, 22 August 2016

    Wataalamu wa takwimu, mawasiliano kukutana Dar


    WATAALAMU wa takwimu, viongozi na wadau mbalimbali wa sekta ya mawasiliano ya simu na benki hapa nchini, watakutana Dar es Salaam kujadili namna wanavyoweza kuvumbua thamani iliyopo kwenye takwimu wanazotumia.
    Mkutano huo wa siku moja umeandaliwa na kampuni ya kuchambua takwimu duniani ya SAS, utakaofanyika Agosti 25, mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kampuni hiyo kuonesha huduma zake kwa miezi miwili ya Agosti na Septemba kwa wadau wa takwimu barani Afrika ikiwemo Tanzania, Ethiopia, Ghana, Nigeria na Kenya .
    “Dunia ya sasa ipo katika mabadiliko ya kitakwimu na uchambuzi wake. Kupitia uzoefu wetu wa takribani miaka 40 kwenye masuala haya, SAS tumekuwa tukiongoza kwenye mabadiliko haya,’’ alisema Meneja Mkuu wa SAS Barani Afrika, Razel Mushiana kupitia taarifa aliyoitoa jana kwa vyombo vya habari.
    Alisema kupitia mkutano huo, kutakuwepo na maonesho yanayohusu uchambuzi wa takwimu unavyoweza kusaidia taasisi kukabiliana na changamoto zilizopo kwenye soko la Afrika na namna zinavyoweza kuvumbua thamani iliyopo kwenye takwimu zao.
    Mushiana alisema, agenda za mkutano huo ni pamoja na majadiliano kuhusu uchambuzi wa takwimu katika kufanya uamuzi, namna ya kujenga utamaduni wa kuchambua takwimu, namna taasisi zinavyoweza kuboresha uzoefu kwa wateja na namna benki zinavyoweza kufanya mageuzi ya kibiashara kupitia uchambuzi wa kina kuhusu hatari (risk)

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI