• Breaking News

    ..

    ..

    Tuesday, 20 September 2016

    DC MUHEZA APIGA MARUFUKU BODABODA KUENDESHWA ZAIDI

     

    Mkuu
    wa wilaya ya Muheza Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza na
    bodaboda wa wilaya hiyo ambapo alikutana nao na kuzungumza nao kwenye
    uwanja wa Jitegemee wilayani humo ambapo alipiga marufuku kuendeshwa
    usiku zaidi ya saa sita.

    Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza
    (Das) akizungumza katika mkutano huo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa
    wilaya hiyo,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo aliyekaa kushoto na anayefuata
    ni Mwenyekiti wa Waendesha Boda Boda wilayani Muheza
     
    Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri
    ya wilaya ya Muheza ambaye pia ni Afisa Biashara wa wilaya hiyo,Ally
    Mokiwa akielezea namna walivyojipanga kuhakikisha waendesha bodaboda hao
    wanakata leseni za kuendesha shughuli zao katikati ni Mkuu wa wilaya ya
    Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo
    wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza, Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo akimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Usalama Barabarani wilayani Muheza(DTO) Herbert Kazonde wakati wa mkutano huo na waendesha bodaboda uliofanyika kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani humo kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza.
    Katibu wa Chama cha Waendesha Boda
    Boda wilayani Muheza,Francis Gerald akizungumza katika mkutano huo
    kuhusu changamoto ambazo zinawakabili
    Baadhi ya waendesha bodaboda
    wilayani Muheza wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi
    Mwanasha Tumbo alipokuwa akizungumza nao kusisitiza umuhimu wa wao kutii
    sheria za usalama barabarani ikiwemo kuacha kufanya vitendo vya uhalifu
    Baadhi ya Bodaboda zikiwa zimepaki kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani Muheza huku madereva wakiwa kwenye kikao chao na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,
    Mhandisi,Hajat Mwanasha Tumbo 

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI