• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 22 September 2016

    DRFA yaipa tano Kili


    CHAMA cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kimeipongeza timu ya taifa ya soka ya wanawake, Kilimanjaro Queens iliyofanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya timu za Afrika Mashariki na Kati, Cecafa ya wanawake iliyofanyika Jinja nchini Uganda.
    Kilimanjaro Queens ambayo inafundishwa na Kocha Mkuu, Sebastian Nkoma na msaidizi wake Edina Lema, ilianza mashindano hayo Septemba 11 na kufanikiwa kuongoza kundi lao na kufanikiwa kutinga fainali na Kenya na kuifunga mabao 2-1.
    Akizungumza na gazeti hili Mwenyekiti wa DRFA, Almasi Kasongo alisema kitendo cha Kilimanjaro Queens kutwaa kombe kinaonesha ni kwa kiasi gani walivyo tayari kupambana kulitangaza taifa.
    “Nawapongeza wachezaji wa Kilimanjaro Queens na benchi la ufundi kwa kutwaa ubingwa wa Cecafa wanawake kwani wameandika historia licha ya kuwa maandalizi yao hayakuwa ya kuridhisha”, alisema Kasongo.
    Pia Kasongo amelipongeza benchi la ufundi kwa uvumilivu mkubwa waliouonesha tangu walipokabidhiwa timu licha ya matayarisho hayakuwa rafiki kiushindani.
    Pia DRFA imeimwagia sifa Serengeti Boys inayosaka tiketi ya kucheza fainali za Vijana za Mataifa ya Afrika chini ya umri wa miaka 17 itakayofanyika mwezi Aprili nchini Madagascar.
    Serengeti Boys imebaki na mchezo moja wa marudiano dhidi ya Congo Brazzaville utakaochezwa Oktoba 2, na ikifanikiwa kuifunga basi watakuwa wamekata tiketi ya kwenda Madagascar.
    Kasongo ameongeza kuwa mafanikio yao ni ya Watanzania wote na kuwaomba wachezaji wasibweteke na hali hiyo na badala yake wazidi kujituma ili kuboresha viwango vyao vya kucheza soka na kulisaidia taifa.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI