• Breaking News

    ..

    ..

    Friday, 16 September 2016

    Mishahara serikalini kuzingatia ujuzi,



    WATUMISHI wa umma kuanzia Februari 2018 wataanza kupangiwa mishahara na posho kulingana na ujuzi na ugumu wa kazi zao.
    Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki amesema serikali inatambua watumishi kutopata mishahara na motisha kulingana na hali na taaluma zao kwa kada mbalimbali nchini.
    Amesema hayo jana wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Tarime, Ester Matiko (Chadema), aliyetaka kufahamu lini serikali itaona umuhimu wa kuwalipa malipo askari magereza nchini kulingana ujuzi wao ili kuwapa motisha kama ilivyo kwa askari wengine.
    Kairuki amesema utaratibu utafanyika kwa watumishi wote wakiwemo askari magereza.
    Amesema hivi sasa ofisi yake imeanza kufanya tathmini ya malipo kwa kada zote na utaratibu huo utakapokamilika kila mtumishi atalipwa malipo yakiwemo ya mshahara na posho kulingana na ujuzi na ugumu wa kazi yake.
    Katika swali la msingi lililoulizwa na Mbunge wa Chumbuni, Ussi Salum Pondeza (CUF), alitaka kufahamu serikali ina mpango gani wa kuwasaidia watumishi kupata haki yao ya vyeo stahiki kama ilivyo kwa wenzao waliopandishwa vyeo.
    Akijibu swali hilo la msingi, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, alisema watumishi wa Idara ya Uhamiaji walioajiriwa mwaka 1999-2000 walikuwa na viwango tofauti vya elimu kama vile kidato cha nne, kidato cha sita, stashahada na shahada kwa watumishi wote hao hakuna aliyefikia cheo cha Kamishna au Kamishna msaidizi kama mbunge alivyouliza.
    Nchemba alisema, watumishi hao kwa sasa wametofautiana vyeo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuajiriwa katika vyeo tofauti kulingana na elimu zao wakati wanaajiriwa na kujiunga katika mafunzo ya awali ya uhamiaji.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI