• Breaking News

    ..

    ..

    Friday, 16 September 2016

    Shahidi akana miamala kesi ya bil.



    SHAHIDI wa 17 katika kesi inayowakabili wafanyakazi 13 wa Benki ya Exim, tawi la Arusha, Abrahamu Shahidi (47), amesema hakufanya miamala ya fedha za kigeni katika benki hiyo wala malipo kwa ajili ya kupeleka watalii katika hifadhi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA).
    Shahidi amesema hayo leo mahakamani wakati akiongozwa na Wakili wa Serikali, Felix Kwetukia, mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha na Arumeru, Deusdedit Kamugisha.
    Amesema mwaka 2012 kwa nyakati tofauti alifanya malipo ya dola 350 na dola 600 katika Benki ya CRDB na siyo benki ya Exim kama alivyooneshwa katika ofisi ya upelelezi ya makosa ya jinai mkoani Arusha.
    Shahidi amesema, ameshangaa kuona jina lake na namba ya simu, kutumika katika kuhamisha dola hizo katika benki ya Exim wakati hakuwahi kufanya malipo katika benki hiyo kwa ajilli ya kupeleka watalii NCAA.
    Shahidi huyo amemtambua mshitakiwa wa 14 katika kesi hiyo, Gervas Lubuva, lakini alikana kufanya naye biashara ya aina yoyote, licha ya jina lake kuonekana katika nyaraka za benki ya Exim.
    Kesi hiyo imehairishwa hadi septemba 19,20,22 na 23 mwaka huu, na serikali inatarajia kupeleka mahakamani hapo mashahidi wengine zaidi.
    Kesi hiyo, inayowakabili wafanyakazi 13 na mshitakiwa mwingine, ni ya kuiba zaidi ya shilingi bilioni saba kwa kughushi, utakatishaji fedha na wizi wa kutumia mfumo wa kibenki.
    Inadaiwa kwamba, washitakiwa hao kwa nyakati tofauti kati ya mwaka 2011 hadi 2012, waliziibia kampuni za utalii na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kughushi nyaraka za akaunti ya dola, fedha za kitanzania na mfumo wa malipo ya kadi.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI