• Breaking News

    ..

    ..

    Friday, 16 September 2016

    MKUU WA MKOA WA SINGIDA AWAASA WAJUMBE WA ALAT KUTATUA KERO

     

    Wakurugenzi, meya na wenyeviti wa halmashauri zote saba Mkoani Singida  wakiendela na katika kikao cha Jumuiya za
    Serikali za mitaa Tanzania (ALAT).
    ……………………………………………………………………………………….
    Na Mwandishi Wetu Singida
    Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe amewaasa
    wakurugenzi, meya na wenyeviti wa halmashauri zote saba Mkoani Singida kutumia
    vikao vya mafuzo ya Jumuiya za Serikali za mitaa (ALAT) kutatua kero za
    halmashauri.
    Mhandisi Mtigumwe ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya ALAT
    mkoa wa Singida na kuwasisitizia kuwa mafunzo hayo yawe na tija na sio kukaa
    vikao visivyo na matokeo chanya.
    Ameongeza kuwa katika kipindi cha miezi sita tangu ateuliwe na
    Mhe Rais amebaini halmashauri zina changamoto za ukusanyaji hafifu na
    usioridhisha wa mapato ya ndani pamoja na mikataba mibovu inayosainiwa na
    halmashauri na hivyo kuiletea hasara serikali.
    Mhandisi Mtigumwe amesema kumekuwa na migogoro ya ardhi
    inayosababishwa na maafisa ardhi wasio kuwa waadilifu, watumishi na madiwani
    kujimilikisha ardhi na vibanda kinyume na utaratibu pamoja na kutotengwa kwa
    asilimia kumi ya mapato ya ndani kwa ajili ya wanawake na vijana.
    “Halmashauri hazijatenga maeneo ya viwanda vidogo na vya kati,
    uchafu umekithiri katika maeneo mengi, watumishi wanaokiuka taratibu
    hawachukuliwi hatua za kinidhamu na mawasiliano hafifu kati ya viongozi na
    watumishi, viongozi na viongozi na hata watumishi wenyewe, hizi ni baadhi ya
    changamoto ambazo kikao cha ALAT kitumike kuzitafutia majibu, alisisitiza.
    Mhandisi Mtigumwe amewasisitiza wakurugenzi kuunda mabaraza ya
    wafanyakazi na halmashauri zenye mabaraza hayo basi vikao vifanyike ili kero na
    changamoto za watumishi zisikilizwe na kutafutiwa ufumbuzi.
    Kwa upande wao meya, wenyeviti na wakurugenzi wa halmashauri
    wamemshukuru mkuu wa Mkoa kwa nasaha alizowapa na kuahidi kuyatumia mafunzo ya
    ALAT katika kuleta mabadiliko katika halmashauri zao.
    Wajumbe walipata fursa ya kujifunza juu ya Mfumo ya serikali za
    mitaa Tanzania bara, ukusanyaji wa mapato ya ndani kwenye halmashauri,
    utaratibu wa manunuzi katika serikali za mitaa , uwazi na uwajibikaji na
    mawasiliano kwa viongozi.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI