• ..

    ..

    Friday, 16 September 2016

    SHEREHE ZA KUFUNGA MAFUNZO YA UONGOZI DARAJA LA KWANZA KOZI NA. 22


     Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
    Rwegasira(katikati) katika Jukwaa akipokea Salaam ya heshima kutoka kwa Gwaride
    la Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi Daraja la Kwanza kozi Na. 22 ya Mwaka
    2016(hawapo pichani) katika hafla ya kufunga Mafunzo hayo leo Septemba 16, 2016
    Chuo cha Magereza, Kiwira Mbeya.
      Kushoto
    ni Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja.
     Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akikagua
    Gwaride la Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi Daraja la Kwanza kozi Na. 22 ya Mwaka 2016.
     Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira
    akimvisha cheo cha Koplo wa Jeshi la Magereza Askari Mhitimu wa Mafunzo hayo kwa niaba ya wenzake.
     Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja(kushoto) katika jukwaa kuu na
    Mgeni rasmi wakifuatilia maonesho mbalimbali ya kujihami askari kama wanavyoonekana katika picha.

    Gwaride la Wahitimu likipita mbele ya jukwaa kwa heshima 
     Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP – John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi kabla ya
    kumkaribisha Mgeni rasmi kutoa hotuba yake ya kufunga rasmi kwa Mafunzo ya
    Uongozi Daraja la Kwanza katika Chuo cha Magereza, Kiwira Mbeya
     Baadhi ya Askari wa Jeshi la Magereza wkichukua matukio mbalimbali kutoka Uwanja wa
    gwaride kama wanavyoonekana.
     Onesho la kijasiri kama inavyoonekana katika picha ambapo mwendesha pikipiki ameweza
    kupita kwa juu usawa wa tumbo huku askari hao wakiwa wamejilaza chini bila uoga.
     Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi Daraja la Kwanza kozi Na. 22 ya Mwaka 2016 wakishangilia
    kwa makofi mara baada ya kufungwa rasmi mafunzo hay oleo Septemba 16, 2016.
     
    (Picha
    zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI