• Breaking News

    ..

    ..

    Monday, 5 September 2016

    Nasha; fursa katika chuo kipya cha kilimo



    WATANZANIA wameshauriwa kutumia fursa zinazopatikana katika chuo kipya cha kilimo cha Borigam, kilichojengwa kwa msaada wa Korea, ili kupata utaalamu zaidi kuhusu kilimo.
    Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa chuo hicho kilichojengwa kwa msaada wa Jumuiya ya Wabudhi katika wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William ole Nasha, alisema kujengwa kwa chuo hicho cha kilimo cha matunda na mboga ni fursa kubwa itakayowezesha kuongeza idadi ya maofisa ugani.
    “Hii ni fursa kwa wakazi wa Kigamboni, Dar es Salaam na Tanzania, tuitumie kuhakikisha tunaongeza wataalamu wengi zaidi katika sekta ya kilimo cha matunda na mboga,” alisema Ole Nasha. Alisema vipo vyuo vya kilimo 14 nchini, lakini vinavyofundisha kilimo cha mboga na matunda ni vichache.
    Alisema nchi inahitaji maofisa ugani 20,000 lakini waliopo ni nusu ya idadi hiyo, hivyo anaamini chuo hicho kimekuja kwa wakati muafaka kutatua changamoto hiyo.
    Mkuu wa chuo hicho kilichopo Mwasonga katika wilaya mpya ya Kigamboni, Joseph Ndunguru, alisema kitasaidia kuzalisha maofisa ugani wengi zaidi katika kilimo cha mboga na matunda.
    Mbali na kutoa mafunzo kwa wanachuo, pia kitatoa mafunzo kwa wanakijiji wa eneo hilo kuhusu kilimo hicho.
    Alisema wamezungumza na uongozi wa shule ya msingi Mkamba uliotoa hekta 10 za ardhi zitakazotumika kama shamba darasa kwa wanafunzi watakaokuwa wakisoma katika chuo hicho na pia kwa wanakijiji kujifunza.
    Alisema kujiunga na chuo hicho ni bure kwa kuwa gharama zote zimelipwa na wafadhili. Alitaja gharama hizo kuwa ni za chakula, malazi na masomo na kuongeza kuwa mwanafunzi atapaswa kulipia mafunzo kwa vitendo pekee

    1 comment:

    1. Hiki Chuo kinapokea wa kuhama kutoka Chuo kingne. Na gharama zote zikoje na jinsi ya malipo inakuaje????

      ReplyDelete

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI