• Breaking News

    ..

    ..

    Monday, 5 September 2016

    CLATTENBURG KUAMUA MANCHESTER DERBY


    clatterburgMark Clattenburg ametangazwa kuwa mwamuzi ambaye atachezesha pambano la wikiendi kati ya mahasimu wawili wa jiji la Manchester, Manchester United na City.
    Pep Guardiola na Mourinho wanakutana kwa mara ya kwanza wakiwa katika vilabu vyenye uhasimu mkubwa bila kusahau uhasama walio nao tangu wakiwa Ligi ya Hispania La Liga.
    Ikumbukwe tu wawili hao hawajapoteza wala kutoa sare hata mchezo mmoja, ikiwa wameanza ligi kwa ushindi wa asilimia 100.
    Manchester City watamkosa mshambuliaji wao tegemezi Sergio Aguero baada ya kufungiwa michezo mitatu kufuatia kumpiga kiwiko beki wa kati wa West Ham Winston Reid.
    Mike Dean ametajwa kama kamishna wa wa mchezo (fourth official), wakati Jake Collins na Steve Bennett watakuwa pembeni kushika vibendera.
    Clattenburg alichezesha fainali ya Uefa Champions League 2015-16 na Euro 2016 na kupewa tena mchezo huu ambao unahesabika kama mchezo wenye ushawishi wa aina yake kwenye ligi ya EPL

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI