• Breaking News

    ..

    ..

    Friday, 23 September 2016

    Nchi tatu zathibitisha Dar


     
    NCHI tatu za Afrika zimethibitisha kuleta wanariadha wake watakaoshindana katika Dar es Salaam Rotary Marathon zitakazofanyika Oktoba 14.
    Kaimu Katibu Mkuu wa Riadha Tanzania (RT), Ombeni Zavalla alisema jana kuwa, maandalizi ya mbio hizo za kila mwaka yanaendelea vizuri.
    Alizitaja nchi hizo zilizothibitisha kushiriki mbio hizo za aina yake kuwa ni pamoja na Ethiopia, Rwanda na Malawi huku Kenya ikitarajia kuthibitisha wakati wowote.
    Zavalla alisema mbio hizo hufanyika Oktoba 14 kila mwaka, ikiwa ni kumbukumbu ya kifo cha rais wa kwanza wa Tanzania Julius Nyerere kilichotokea tarehe hiyo.
    Dar Rotary marathon ni za kilometa 21 na kila mwaka zimekuwa na mafanikio makubwa kwa kushirikisha wanariadha nyota kutoka ndani ya nje ya Tanzania na washindi kupewa zawadi nono.
    Kwa miaka kadhaa, Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amekuwa mgeni rasmi wa mbio hizo kwa kushiriki zile za kilometa tano na viongozi wengine.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI