KAMPUNI ya SBC Tanzania Limited inayotengeneza vinywaji baridi imekabidhi madawati 200 yenye thamani ya Sh milioni 22 kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, ikiwa ni mwendelezo wa jitihada za kampuni hiyo kuitikia mwito wa serikali kuchangia madawati kwa ajili ya kumaliza kabisa matatizo ya madawati shuleni.
Akizungumza wakati wa makabidhiano katika Shule ya Msingi Gogo iliyoko Chanika, Mjema aliwaagiza watendaji wake kuhakikisha madawati wanayoendelea kuyapokea kutoka kwa wadau mbalimbali yanaelekezwa kwenye shule mpya na za zamani zenye mahitaji.
“Nawapongeza SBC Tanzania Limited kwa kuendelea kutuchangia madawati. Hili jambo ni jema kwa sababu kampuni hii imeona ni muhimu watoto wetu ambao wako Wilaya ya Ilala wapate madawati na kusoma katika mazingira bora,”alisema na kuongeza kuwa watakapopata elimu bora na kujiajiri watatoa ajira kwa wengine.
Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa SBC Tanzania Limited (PEPSI), Avinash Jha, alisema kampuni hiyo inatambua changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta ya elimu nchini, ndio maana wameipa umuhimu elimu katika sera yao ya kuisaidia jamii.
“Mwezi uliopita kampuni yetu kupitia tawi la Shinyanga ilichangia Sh milioni 20 kwa ajili ya kusaidia kutengeneza madawati kwa shule za mkoa wa Shinyanga.
No comments:
Post a Comment