• Breaking News

    ..

    ..

    Friday, 16 September 2016

    WATU TANO WANAODAIWA MAJAMBAZI WAKAMATWA


     Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akizungumza na waandishi wa Habari juu
    opreresheni ambazo zimefanyika na mafanikio yake leo jijini Dar es Salaam.
     Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha Bunduki aina ya Gobole kwa
    waandishi habari jijini Dar es Salaam. 
    04.Kamanda wa Polisi Kanda Maalu
    Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyeshaBastola
    aina ya Browning TZCAR No.87881 kwa waandishi habari jijini Dar es Salaam.
     Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha namba za usajili bandia zinazotumiwa na wahalifu pikipiki kwa waandishi habari jijini Dar es Salaam.
    Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha magari yaliyoibiwa sehemu mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam 1 kwa waandishi habari jijini Dar es Salaam.
                (Picha na Emmanuel Massaka,Globu jamii)
    …………………………………………………………………………………………
    Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
     
    Kikosi Maalum cha Kupambana na ujambazi wa kutumia silaha cha Polisi Kanda Maalum ya
    Dar Es salaam kimefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watano kwa makosa ya ujambazi
    wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar Es salaam.
    Akizungumza
    na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Kamada wa Polisi wa Kanda Maalum,
    Kamishina Simon Sirro amesemaa askari Polisi wakiwa katika ufuatiliaji maeneo
    ya Goba Wilaya ya kipolisi Kawe Mkoa wa Kinondoni walimkamata mwanamke mmoja mkazi wa Goba, baada ya kupata taarifa
    kuwa anawafahamu majambazi wanaojihusisha na uvamizi kwenye maduka makubwa.
    Amesema
    Katika na mwanamke huyo mahojiano aliwataja washirika wake watano  ambao walifuatiliwa na kukamatwa katika
    upekuzi walipatikana na silaha moja Bastola aina ya Browning TZCAR No.87881 ikiwa na risasi 17.
    Sirro
    amesema katika mahojiano zaidi watu hao walikiri kufanya matukio ya ujambazi wa
    kutumia silaha jijin Dar es Salaam na mmoja wao alitaja silaha  nyingine amezifichwa kwenye majaruba ya
    Chumvi maeneo ya Ununio na kuwaongoza askari hadi kwenye eneo husika.
    walipofika maeneo hayo mtuhumiwa alianza kukimbia kuelekea kichakani ndipo
    Askari walirusha risasi iliyompata mguu wa kushoto  na kufanikiwa kumkamata.
    Hata
    hivyo mtuhumiwa alifariki akiwa njiani kuelekea hosptalini kutokana na kuvuja
    damu nyingi kutokana na jeraha la risasi.
    Aidha
    kati ya watuhumiwa wengine waliobaki mmoja aliwaongoza askari hadi eneo la
    gongolamboto anakoishi ambapo katika upekuzi
    alipatikana
    silaha nyingine aina ya Shotgun Pump
    action ambayo imefutwa namba za usajili, msumeno mmoja na tupa moja  ya kunolea misumeno na visu.
    Watuhumiwa wote wanne wanaendelea kuhojiwa mara ya
    upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani.
    Katika tukio
    lingine Polisi kanda Maalum Dar es salaam huko magomeni mtaa wa
    makumbusho  askari wakiwa doria  waliwatilia mashaka watu wawili wakiwa
    wamepakizana kwenye Pikipiki na begi dogo mgongoni ndipo askari
    waliwasimamisha
    hawakutii amri hiyo, Polisi walifuatilia ili kuwahoji  lakini watu hao
    baada ya kugundua kuwa Polisi
    wanawafuatilia walianza kukimbia kwa kasi mara wakatupa begi hilo,
    askari
    waliliokota baada ya  kulipekua begi hilo
    walikuta Bastola mbili aina ya Browning No, NE984517CAT5802  Ikiwa na
    risasi 11 na nyigine yenye No. CZ
    2075 aina ya RAMI ikiwa na risasi 21 na magazine mbili iliyotengenezwa
    CZECH
    REPUBLIC jitihada ya kuwasaka watu hao zinaendelea.
    Kamishna
    wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam anatoa wito kwa Wenyeviti wa serikali
    za mitaa kupitia kamati za ulinzi na usalama za mitaa kuimarisha ulinzi na
    usalama  katika maeneo yao na kutimiza
    wajibu wao, amewataka wamiliki wote wa nyumba jijini kuhakikisha kuwa wanaweka
    kipengele cha kuwepo na picha katika mikataba ya kupangisha nyumba zao kutokana
    na uwepo wa wimbi la uhalifu jijini.
    Aidha
    amewataka kufuatilia jambo hilo kwa ukaribu ikiwa ni pamoja na wao kuwa na
    picha za wapangaji wa nyumba hizo, kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kuweza
    kuwabaini wahalifu mbalimbali katika maeneo yao, atakayeshindwa kutekeleza
    wajibu wake atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kupelekwa mahakamani.
    Kikosi Maalum cha Kupambana na wezi wa
    magari cha Polisi Kanda Maalum Dar Es Salaam ililipokea taarifa toka kwa raia
    mwema kuwa kuna gari aina ya Toyota Carina T 289 DFL imeibiwa jijini DSM maeneo
    ya Kimara na kupelekwa mafichoni Mjini Mbeya. Baada ya taarifa hizo kupokelewa ndipo
    ufuatiliaji ulianza na  mtuhumiwa Mzawari
    Ahmad (29) mkazi wa mwananyamala alikamatwa jijini MBEYA akiwa na wenzake  wawili na alikiri kuhusika na tukio hilo.
    Jeshi
    la polisi lilipata  taarifa toka kwa raia mwema kwamba huko Mkoa wa
    Kilimanjaro kuna gari nyingine aina ya Suzuki Carry T234 DAJ ambayo
    iliibwa
    maeneo ya Tandale jijini DSM mali ya NURDIN MPELEMBE. Askari walisafiri
    mkoa tajwa
    tarehe 05/09/2016 na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa Serafin
    Valerian(46),
    mfanyabiashara, mkazi wa Himo Kilimanjaro akiwa na magari  matatu ya
    wizi nyumbani kwake. Magari hayo ni:  SUZUKI CARRY T935 CPC rangi nyeupe
    namba zake
    halisi ni T139 DEK mmiliki ni BRAYAN LYIMO wa Ilala mtaa wa Arusha Dsm,
    gari
    nyingine ni TOYOTA RAV 4 rangi ya silver T732 CHP ambayo iliibwa kimara
    jijini
    Dsm tarehe 11/01/2016 nyumbani kwa CECULAR JAMES LAURICH namba halisi ni
    T440CAW.
     Mtuhumiwa  baada ya kupekuliwa alipatikana na hati
    mbalimbali za magari na pikipiki ambazo ni: kadi za bajaji, bima za magari
    mbalimbali yaliyopata ajali na kulipwa, plate namba za pikipiki, motorvehicle
    licence na TIN namba zenye majina mbalimbali.
    watuhumiwa wote wakiwemo madalali wa magari haya ya wizi wanaendelea
    kutafutwa na mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa kwa mahojiano mara upelelezi
    utakapokamilika atapelekwa mahakamani.
    polisi kanda maalum d’salaam yakusanya milioni tsh
    882,570,000
    /= tozo za makosa ya usalama barabarani kuanzia
    Septemba 6 hadi septemba 16.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI