• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday, 26 October 2016

    CHUMI ZA AFRIKA ZAPITISHA IDADI KUBWA ZAIDI YA MAGEUZI YA KIBIASHARA

                                                            BENKI YA DUNIA


    WASHINGTON, Octoba,2016- Uchumi wa nchi za Afrika kusini ya sahara zimefanya idadi kubwa zaidi ya mageuzi katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita ili kuboresha mazingira ya biashara kwa wajasiriamali wenyeji, linasema toleo la mwaka la ripoti ya kufanya bishara ya benki ya Dunia.


    Kufanya Biashara 2017; Fursa sawa kwa wote ripoti iliyotolewa leo inaeleza kwamba chumi 37 kati ya chumi 48 za kanda zilipitisha mageuzi 80 katika kipindi cha mwaka uliopita, Ongezeko la asilimia 14 kutoka mwaka uliopita. Zaidi ya nusu ya mageuzi ya mwaka jana yalitekelezwa na wanachama 17 wa shirika usawazishaji wa Sheria ya Biashara katika Afrika (OHADA)


    Chumi za kanda zilifanya mageuzi zaidi katika maeneo ya kutatua Ufilisi (ikiwa na mageuzi 18) na katika kuanzisha biashara (15). Nigeria, Rwanda na Afrika ya kusini kwa mfano, zilifanya kuanzisha biashara kuwa brahisi zaidi kwa kuanzisha au kuboresha maombi kupitia mitandao. Aidha kama sehemu ya ajenda ya mageuzi ya OHADA nchi ya Cameroon, pamoja na mambo mengine, ilianzisha utaratibu mpya wa kusuluhisha makampuni ambayo yako kwenye matatizo ya fedha. Hii hufanya sasa kutatua ufilisi kuwa rahisi zaidi kwa kuruhusu njia za ziada za kulipa madeni.


    Chumi katika nchi 7 zilitekeleza mageuzi yanayohusiana na kufanya biashara baina ya mipaka. Kwa mfano, Niger ilifanya biashara inayovuka mipaka kuwa rahisi zaidi kwa kuondoa sharti la ukaguzi wa lazima kabla ya kusafirisha mzigo wa bidhaa zilizoingizwa nchini. Pia mauritania ilifanya biashara inayovuka mipaka kuwa rahisi zaidi kwa kuanza kutumia mfumo wa kimataifa wa kubadilishana data za kielektoniki ASYCUDA ambao unapunguza muda wa kutayarisha na kuwasilisha fomu za forodha kwa bidhaa zinazosafilishwa nje ya bidhaa zinazoingizwa nchini. kwa mfano,inachukua siku 51 tu mjini Nouakchott, Mauritania kukamilisha taratibu za nyaraka kwa ajili ya kusafirisha bidhaa nje, ukilinganisha na siku 59 huko nyuma.


    Kadri serikali nyingi zinavyoendelea kutekeleza ajenda ya mageuzi,data kutoka ripoti ya 'kufanya biashara'inaonyesha mafanikio yanayoendelea katika nchi hizo, kwa mfano inachukua siku 27 kuanzisha biashara katika nchi za Afrika kusini ya sahara, ikilinganishwa na siku 37 miaka mitano iliyopita.


    Pia pamoja na hayo kiashiria cha kulipa kodi kimepanuliwa ili kijumuishe michakato baada ya kukabidhi fomu za kodi, kama vile ukaguzi wa hesabu za kodi na marejesho ya VAT. Ripoti imegundua kwamba kanda ina nafasi ambayo kuna uwezekano wa ukaguzi wa hesabu kufanyika-walipa kodi wanakutana na ukaguzi wa maeneo yao ambapo mkaguzi wa hesabu huwatembelea walipa kodi. Hivyo ndivyo ilivyo kwa nchi za Botswana,Gambia,Malawi na Zimbabwe.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI