• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday, 26 October 2016

    HATIMAE TANZANIA YAFANYA MAONYESHO YA VIWANDA

      WIZARA YA VIWANDA
                   
    Wizara ya viwanda, bishara na uwekezaji kupitia taasisi yake ya mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania (TanTrade) inawakaribisha watanzania wote wanaomiliki viwanda vidogo, vyakati na vikubwa kushiriki maonesho ya viwanda vya Tanzania yatakayofanyika kuanzia tarehe 7 hadi 11 katika uwanja wa maonyesho wa Mwalimu  j.k.Nyerere, Barabara ya Kilwa, Dar es salaam.


    Lengo kuu la maonyesho haya ni kujenga jukwaa kwa wadau wa sekta ya viwanda kupata fursa ya kujadiliana, kubadilishana uzoefu na kutangaza fursa zilizopo katika sekta hii, Aidha maonyesho haya yatatoa fursa nyingine.


    Hata hivyo Waziri wa viwanda, Biashara na Uwekezaji MH. CHARLES J.P.MWIJAGE (MB) AmasemaMaonyesho haya yanabeba kauli mbiu isemayo ''TANZANIA SASA TUNAJENGA VIWANDA '' ikilenga
    kuwaaminisha wananchi juu ya falsafa na dhima ya ujenzi wa uchumi wa viwanda. Chini ya kaulimbiu hii tunawahamasisha Watanzania wathubutu kujenga viwanda kwa kuwakutanisha na wale
    waliokwisha anza siku nyingi, lakini na wale walioanza kipindi kifupi kilichopita. Tutaendelea na kampeni ya kuthamini, kupenda na kununua bidhaa zizalishwazo nchini, lakini pia kuwasiliwazalishaji bidhaa zenye viwango vya hali ya juu
    .

    Katika maonyesho haya tunalenga kuwakutanisha wadau wote wa viwanda. Hawa ni pamoja wazalishaji wa malighafi, taasisi zinazotoa huduma kwa wenye viwanda na taasisi zinazowezesha bidhaa kutoka kiwandani mpaka kufikia mikononi mwa watumiaji. Kama mnavyojua mpango wa pili wa miaka mitano unatamka wazi kuwa sekta binafsi ndiyo mhimili wa ujenzi wa uchumi wa viwanda. Hivyo maonyesho haya mhusika mkuu ni sekta binafsi na serikali sisi ni wawezeshaji.


    Ili kushiriki maonyesho haya tafadhali tembelea ofisi za mamlaka ya maendeleo ya biashara ya Tanzania (TanTrade) zilizopo katika uwanja wa maonyesho ya biashara ya Mwl. j.k.Nyerere, Barabaraya kilwa Dar es salaam ambao ni waratibu wa maonesho haya kupitia kamati ya maandalizi ya kitaifa ya maonesho ya viwanda vya tanzania na kusimaamiwa na ofisi ya waziri mkuu na wizara ya viwanda, Biashara na uwekezaji na Taasisi ya umoja wa mataifa ya maendeleo ya viwanda (UNIDO)

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI