• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 20 October 2016

    KONGAMANO LA NNE GESI NA MAFUTA LAFANYIKA JIJINI DAR

    m1
    Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo (kushoto) akifugua kongamano la nne linalohusu gesi na mafuta lililoambatana na maonesho , lililokutanisha wadau mbalimbali kutoka makampuni yanayohusika na utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi, vyuo  vikuu, wizara na  taasisi za serikali jijini Dar es Salaam.
    m2
    Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo (kushoto), akibadilishana mawazo na  Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, James Andilile (kulia) katika kongamano hilo
    m3
    Kutoka kulia; mwakilishi kutoka Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET), Profesa Abraham Temu, Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, James Andilile na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa katika kongamano hilo.
    m4
    Washiriki kutoka makampuni yanayohusika na utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi, vyuo  vikuu, wizara na  taasisi za serikali wakifuatilia hotuba iliyokuwa inatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo (hayupo pichani) katika kongamano hilo.
    m5
    Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Kapuulya Musomba (kushoto) akipokea tuzo kutoka  kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo (kulia)  kwa mchango  wa shirika  hilo katika  kufanikisha kongamano  hilo.
    m6
    Mwakilishi kutoka Benki ya Standard Chartered, Thomas Bisonga (kushoto) akipokea tuzo kutoka  kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo (kulia)  kwa mchango  wa benki hiyo katika  kufanikisha kongamano  hilo.
    m7
    Mwakilishi kutoka kampuni inayojihusisha na ujenzi wa mabomba ya gesi kutoka China (kushoto) akipokea tuzo kutoka  kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo (kulia)  kwa mchango  wa  kampuni hiyo katika  kufanikisha kongamano  hilo.
    m8
    Meneja Mawasiliano kutoka kampuni ya utafiti na uchimbaji wa gesi na mafuta nchini ya Statoil, Genevieve Kasanga (kushoto), akipokea tuzo kutoka  kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo (kulia)  kwa mchango  wa  kampuni hiyo katika  kufanikisha kongamano  hilo.
    m9
    Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Kapuulya Musomba akieleza jambo katika kongamano hilo.
    m10
    Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo (katikati waliokaa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya washiriki wa kongamano hilo.

    Na Greyson Mwase, Dar es Salaam
    Kongamano la Nne linalohusu sekta ndogo ya mafuta na gesi lililoambatana na maonesho  kuhusu sekta hiyo na kukutanisha   Wadau mbalimbali ikiwemo Kampuni zinazojishughulisha na utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi, Vyuo Vikuu, Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali  limeanza kufanyika jijini  Dar es Saalaam.
    Kongamano hilo lilifunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo ambapo aliwaeleza wadau hao kuwa, usimamizi madhubuti wa sekta ndogo ya gesi na mafuta utaleta  mapinduzi makubwa kwenye  ukuaji  wa viwanda na kuiwezesha Tanzania  kuingia kwenye  uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
    Katika kongamano hilo linalofanyika kuanzia tarehe 20 – 21 Oktoba, 2016, Dk. Pallangyo alisema kuwa kutokana na kiasi kikubwa cha gesi  kilichogunduliwa ambacho ni  futi za ujazo trilioni 57.2, kampuni mbalimbali za kigeni zimeanza kujitokeza na kuwekeza katika mikoa  ya Lindi na Mtwara ambapo gesi imegunduliwa
    Alisema kutokana na  uwekezaji  katika  shughuli za gesi na mafuta, kumekuwepo na mabadiliko ya kiuchumi katika mikoa hiyo kama  vile  kuongezeka kwa fursa za ajira, malazi na utoaji wa huduma kwa wawekezaji.
    Aliongeza kuwa ni vyema wananchi  hususan wa maeneo hayo kujiandaa na uwekezaji mkubwa katika mikoa hiyo  ambapo kwa sasa katika mikoa ya Lindi na Mtwara kunatarajiwa kujengwa  viwanda  vikubwa vya mbolea, vitakavyoleta neema katika mikoa hiyo.
    Alisema katika kujiandaa na kasi ya  ukuaji wa  sekta za  gesi na mafuta nchini  serikali imeweka mikakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na  kuhakikisha kunakuwepo na sera na sheria zitakazowezesha wazawa kuwa sehemu ya umiliki wa uchumi  wa gesi na mafuta.
    Alitaja mikakati mingine ni pamoja na uanzishwaji wa kozi zinazohusu masuala ya  gesi na mafuta katika  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam  (UDSM) na  Chuo Kikuu cha  Dodoma (UDOM).
    Aliongeza kuwa, Serikali imekuwa ikipeleka nje ya nchi  kusomea masuala ya  gesi na mafuta katika ngazi ya shahada ya uzamili (masters degree), wanafunzi wanaofanya  vizuri  kwenye masomo  ya sayansi  katika ngazi ya shahada.
    “Lengo letu kama Serikali ni kuhakikisha  Tanzania inakuwa na wataalam wa kutosha  watakaoshiriki katika uchumi wa gesi na mafuta kwa kuajiriwa kwenye makampuni yanayojihusisha na  utafiti na uchimbaji  wa  gesi na mafuta,” alisema Dk. Pallangyo.
    Wakati huo huo akizungumza katika kongamano hilo, mwakilishi kutoka Taasisi ya  Wahandisi  Tanzania (IET), Profesa Abraham Temu alisema kuwa lengo la kongamano hilo  lilikuwa ni kujadili  na kubadilishana uzoefu kuhusu sekta za gesi na mafuta nchini.
    Alisema mambo yatakayojadiliwa katika kongamano  hilo ni pamoja na uelewa kuhusu sekta za  gesi na mafuta,  sera na sheria za mafuta na gesi, ushirikishwaji wa wazawa kwenye sekta za  gesi na mafuta,  changamoto na matumizi endelevu ya mafuta na gesi na rushwa.
    Kongamano hilo  liliandaliwa na  Wizara  ya Nishati na Madini kwa kushirikiana na  Taasisi ya Wahandisi  Tanzania (IET),  Shirika la Maendeleo  ya Petroli Tanzania (TPDC), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na  Chuo Kikuu cha  Dar es Salaam (UDSM

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI