• Breaking News

    ..

    ..

    Monday, 24 October 2016

    MAMELODI SUNDOWNS YATWAA TAJI LA KLABU BINGWA AFRIKA 2016 MJINI CAIRO.


    Historia imeandikwa usiku wa jana na timu ya Mamelodi Sundown’s kwa kutwaa taji la klabu bingwa Afrika kwa mwaka 2016 licha ya kufungwa bao 1-0 na wenyeji Zamalek ya Misri katika uwanja wa Alexandria na ikumbukwe mwaka jana TP Mazembe ndio walichukua.

    Matokeo hayo yanaifanya Sundowns kushinda kwa jumla ya  magoli 3-1 baada ya kushinda mchezo wa awali wa magoli 3-0 huko e Afrika Kusini Jumamosi iliyopita na kuanza kuwapoteza waarabu kimya kimya kisoka hii inatokana na timu za watu wenye asili ya weusi kuanza kufanya vizuri.

    Hata hivyo hili Taji la kwanza kwa klabu hiyo ya Afrika Kusini ambayo fainali yake ya mwisho katika michuano hiyo ilikuwa ni 2001 ambapo ilipoteza mbele ya Al Ahly ambao ni mahasimu wakubwa wa Zamalek.

    Zamalek walipata goli lao la pekee dakika ya 62 kutoka kwa Stanley Ohawuchi licha ya kutawala mchezo huo kwa asilimia kubwa huku

    Sundowans wakicheza kwa kushambulia wakati wote licha ya kuwa wenyeji kutaka kupata magoli zaidi.

    Baada ya kusema mashabiki 20,000 pekee ndio watakaoruhusiwa kushuhudia pambano hilo kwa sababu za kiusalama, mamlaka ya Misri waliruhusu mashabiki 86,000 kuingia uwanjani kushuhudia mtanange huo ili kutoa support kwa timu yao.

    Kwa matokeo hayo Sundown’s imevunja rekodi mbovu za timu za Afrika Kusini kufungwa na waarabu na ikumbukwe msimu zimekutana mara tatu kwenye makundi Sundown’s waliwafunga Zamalek nje ndani wakianza Cairo 2-0 na A.Kusini 2-1,Fainali ya kwanza Zamelek alifungwa 3-0 na marudiano Sundown’s kachapwa 1-0.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI