• Breaking News

    ..

    ..

    Monday, 24 October 2016

    WAKATI MZAMBIA AKICHUKUA MIKOBA PLUIJM KUPANDISHWA CHEO

    Huku timu ya Yanga ikililia mabadiliko jana uliwashtusha watu wengi kwa kutua kwa Kocha Mkuu wa timu ya Zesco United,George Lwandamina raia wa Zambia, kuja kumalizana na uongozi wa klabu hiyo na atachukua mikoba ya babu mwenye rekodi ya kipekee Tanzania,Hans Van Der Pluijm .

    Taarifa zimeeleza kwamba kocha huyo ametua mchana na amewekwa katika moja ya hoteli kubwa jijini Dar es Salaam, Yanga wakitaka kufanya siri kubwa.

    Kamati ya Ufundi ya Yanga, imempendekeza kocha huyo kutua nchini na kuinoa Yanga badala ya Kocha Hans van der Pluijm.

    Hata hivyo, taarifa nyingine zimeeleza kocha huyo anaweza kuchukua nafasi ya Pluijm ambaye atakuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Yanga.

    Bado kumekuwa na mkanganyiko kuhusiana na kocha huyo kwa kuwa Yanga wamefanya ni siri kubwa.

    Lakini habari za uhakika zimeeleza, tayari Yanga wamemalizana naye licha ya kuwa wanafanya siri kubwa kuhusiana naye.

    “Kila kitu kimemalizika, kocha yuko Dar es Salaam, mambo yanakwenda safi kabisa. Lakini vuteni subira,” alisema mpasha taarifa.

    Lwandami alikuwa kocha bora wa Zambia msimu wa 2014-15, pia aliwahi kuinoa Zesco ya Zambia kwa mafanikio makubwa, pia timu ya taifa ya Zambia maarufu kama Chipolopolo.

    Mwaka huu ameweza kuifikisha kwenye hatua ya nusu fainali timu ya Zesco United na kutolewa na Mamelodi Sundown’s ambao jana usiku wametwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika CAF kwa kuwatwanga Zamelek 3-1.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI