Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania na pia ni Nahodha anayechezea Ubelgiji kwenye Klabu ya KRC Genk ameisaidia kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wageni Sint-Truiden mchezo wa Ligi Kuu ya Ubelgiji.
Sint-Truiden waliwabana vilivyo washambuliaji wa Genk wakiongozwa na Samatta pamoja na kinda wa kijapani Leon Bailey na kushindwa kuipenya kirahisi ngome ya wageni hadi timu hizo zinakwenda mapumziko zilikuwa bado hazijafungana.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kushambulia kwa kasi na kusaka bao la kuongoza huku zikifanya mabadiliko kwa lengo la kuimarisha safu zao ili ziweze kuibuka na ushindi muhimu wa Ligi hiyo.
Genk walifanya mabadiliko kwa kuwatoa,Tino-Sven Susic dk 46,Leandro Trossard 62 na Leon Bailey 78 na nafasi zao kuchukuliwa na Nikos Karelis,Thomas Buffel pamoja na Bryan Heynen wakati wapinzani wao waliwatoa Jonathan Bamba dk 75 na Yohan Boli dk ya 68 na mabadiliko hayo yaliwanufaisha wenyeji.
Akitokea benchi Nikos Karelis aliifungia goli la ushindi Genk zikiwa dakika za jioni 88 na kuwafanya mashabiki waliokuwa wamefurika katika uwanja huo kulipuka kwa shangwe na hadi mpira unamalizika Genk wameibuka na ushindi wa 1-0.
Kwa matokeo hayo Genk wanapanda mpaka nafasi ya saba ya msimamo wa Ligi ya Ubelgiji wakiwa na pointi 17 wakati Sint-Truiden wakishuka hadi nafasi ya 13 kwa pointi 9.
No comments:
Post a Comment